ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
96 : 7

وَلَوۡ أَنَّ أَهۡلَ ٱلۡقُرَىٰٓ ءَامَنُواْ وَٱتَّقَوۡاْ لَفَتَحۡنَا عَلَيۡهِم بَرَكَٰتٖ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَٰكِن كَذَّبُواْ فَأَخَذۡنَٰهُم بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ

Na lau kuwa watu wa miji wangeliamini na wakamcha Mungu, basi hakika tungeliwafungulia baraka za kutoka mbinguni na ardhi. Lakini walikadhibisha, basi tukawachukua kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma. info
التفاسير:

external-link copy
97 : 7

أَفَأَمِنَ أَهۡلُ ٱلۡقُرَىٰٓ أَن يَأۡتِيَهُم بَأۡسُنَا بَيَٰتٗا وَهُمۡ نَآئِمُونَ

Je, wakazi wa vijijini wana amani ya kuwa iwajie adhabu yetu usiku hali ya kuwa wamelala? info
التفاسير:

external-link copy
98 : 7

أَوَأَمِنَ أَهۡلُ ٱلۡقُرَىٰٓ أَن يَأۡتِيَهُم بَأۡسُنَا ضُحٗى وَهُمۡ يَلۡعَبُونَ

Au wakazi wa vijijini wana amani ya kuwa iwajie adhabu yetu mchana hali ya kuwa wanacheza? info
التفاسير:

external-link copy
99 : 7

أَفَأَمِنُواْ مَكۡرَ ٱللَّهِۚ فَلَا يَأۡمَنُ مَكۡرَ ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡقَوۡمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ

Je, wana amani dhidi ya mipango ya Mwenyezi Mungu? Kwani hawawi na amani dhidi ya mipango ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kaumu waliohasiri. info
التفاسير:

external-link copy
100 : 7

أَوَلَمۡ يَهۡدِ لِلَّذِينَ يَرِثُونَ ٱلۡأَرۡضَ مِنۢ بَعۡدِ أَهۡلِهَآ أَن لَّوۡ نَشَآءُ أَصَبۡنَٰهُم بِذُنُوبِهِمۡۚ وَنَطۡبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَسۡمَعُونَ

Kwani haijawabainikia wale wanaoirithi ardhi baada ya wale wenyewe kwamba tukitaka tunawasibu kwa madhambi yao, na tukaziba nyoyo zao, kwa hivyo hawatasikia? info
التفاسير:

external-link copy
101 : 7

تِلۡكَ ٱلۡقُرَىٰ نَقُصُّ عَلَيۡكَ مِنۡ أَنۢبَآئِهَاۚ وَلَقَدۡ جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَمَا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُواْ بِمَا كَذَّبُواْ مِن قَبۡلُۚ كَذَٰلِكَ يَطۡبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Vijiji hivyo, tunakusimulia katika habari zake. Na hakika waliwajia Mitume wao na hoja zilizo waziwazi. Lakini hawakuwa wenye kuamini yale waliyoyakadhibisha zamani. Namna hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyoziba kwenye nyoyo za makafiri. info
التفاسير:

external-link copy
102 : 7

وَمَا وَجَدۡنَا لِأَكۡثَرِهِم مِّنۡ عَهۡدٖۖ وَإِن وَجَدۡنَآ أَكۡثَرَهُمۡ لَفَٰسِقِينَ

Wala hatukuwapata wengi wao wakiwa ni wenye ahadi yoyote, bali kwa hakika tuliwapata wengi wao ni wavukao mno mipaka. info
التفاسير:

external-link copy
103 : 7

ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِم مُّوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ فَظَلَمُواْ بِهَاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُفۡسِدِينَ

Kisha tukamtuma baada yao Musa na Ishara zetu kwa Firauni na waheshimiwa wake. Nao wakazifanyia dhuluma. Basi tazama namna ulivyokuwa mwisho wa waharibifu. info
التفاسير:

external-link copy
104 : 7

وَقَالَ مُوسَىٰ يَٰفِرۡعَوۡنُ إِنِّي رَسُولٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na Musa akasema, "Ewe Firauni! Hakika mimi ni Mtume kutoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote " info
التفاسير: