ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
66 : 4

وَلَوۡ أَنَّا كَتَبۡنَا عَلَيۡهِمۡ أَنِ ٱقۡتُلُوٓاْ أَنفُسَكُمۡ أَوِ ٱخۡرُجُواْ مِن دِيَٰرِكُم مَّا فَعَلُوهُ إِلَّا قَلِيلٞ مِّنۡهُمۡۖ وَلَوۡ أَنَّهُمۡ فَعَلُواْ مَا يُوعَظُونَ بِهِۦ لَكَانَ خَيۡرٗا لَّهُمۡ وَأَشَدَّ تَثۡبِيتٗا

Na lau kuwa tuliwaandikia kuwa: Jiueni, au tokeni majumbani mwenu, wasingeliyafanya hayo isipokuwa wachache tu miongoni mwao. Na lau kama wangeliyafanya yale wanayowaidhiwa kwayo, ingelikuwa bora kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi. info
التفاسير:

external-link copy
67 : 4

وَإِذٗا لَّأٓتَيۡنَٰهُم مِّن لَّدُنَّآ أَجۡرًا عَظِيمٗا

Na hapo tungewapa malipo makubwa kutoka kwetu. info
التفاسير:

external-link copy
68 : 4

وَلَهَدَيۡنَٰهُمۡ صِرَٰطٗا مُّسۡتَقِيمٗا

Na tungeliwaongoa njia iliyonyooka. info
التفاسير:

external-link copy
69 : 4

وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ فَأُوْلَٰٓئِكَ مَعَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِم مِّنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ وَٱلصِّدِّيقِينَ وَٱلشُّهَدَآءِ وَٱلصَّٰلِحِينَۚ وَحَسُنَ أُوْلَٰٓئِكَ رَفِيقٗا

Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume, basi hao wako pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi (Wakweli), na Mashahidi, na Watu wema. Na hao ndio wenza wazuri mno! info
التفاسير:

external-link copy
70 : 4

ذَٰلِكَ ٱلۡفَضۡلُ مِنَ ٱللَّهِۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ عَلِيمٗا

Hiyo ndiyo fadhila itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kwamba ndiye Mwenye kujua. info
التفاسير:

external-link copy
71 : 4

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ خُذُواْ حِذۡرَكُمۡ فَٱنفِرُواْ ثُبَاتٍ أَوِ ٱنفِرُواْ جَمِيعٗا

Enyi mlioamini! Chukueni tahadhari yenu! Na mtoke haraka kwa vikosi au tokeni nyote kwa pamoja! info
التفاسير:

external-link copy
72 : 4

وَإِنَّ مِنكُمۡ لَمَن لَّيُبَطِّئَنَّ فَإِنۡ أَصَٰبَتۡكُم مُّصِيبَةٞ قَالَ قَدۡ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيَّ إِذۡ لَمۡ أَكُن مَّعَهُمۡ شَهِيدٗا

Na hakika yupo kati yenu anayejikokota sana. Na ukiwapata (nyinyi) msiba, husema: Hakika Mwenyezi Mungu amenineemesha kwa vile sikuwa nimehudhuria pamoja nao. info
التفاسير:

external-link copy
73 : 4

وَلَئِنۡ أَصَٰبَكُمۡ فَضۡلٞ مِّنَ ٱللَّهِ لَيَقُولَنَّ كَأَن لَّمۡ تَكُنۢ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُۥ مَوَدَّةٞ يَٰلَيۡتَنِي كُنتُ مَعَهُمۡ فَأَفُوزَ فَوۡزًا عَظِيمٗا

Na ikiwapata fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu, anasema, kana kwamba hapakuwa mapenzi baina yenu na yeye: Aa! Laiti ningelikuwa pamoja nao nikafuzu kufuzu kukubwa. info
التفاسير:

external-link copy
74 : 4

۞ فَلۡيُقَٰتِلۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱلَّذِينَ يَشۡرُونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا بِٱلۡأٓخِرَةِۚ وَمَن يُقَٰتِلۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَيُقۡتَلۡ أَوۡ يَغۡلِبۡ فَسَوۡفَ نُؤۡتِيهِ أَجۡرًا عَظِيمٗا

Basi na wapigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu wale ambao wanauza uhai wa dunia kwa Akhera. Na mwenye kupigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, kisha akauwawa au akashinda, basi tutampa ujira mkubwa. info
التفاسير: