ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
45 : 4

وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِأَعۡدَآئِكُمۡۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَلِيّٗا وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ نَصِيرٗا

Na Mwenyezi Mungu anawajua vyema maadui zenu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mlinzi, na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mwenye kunusuru. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 4

مِّنَ ٱلَّذِينَ هَادُواْ يُحَرِّفُونَ ٱلۡكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِۦ وَيَقُولُونَ سَمِعۡنَا وَعَصَيۡنَا وَٱسۡمَعۡ غَيۡرَ مُسۡمَعٖ وَرَٰعِنَا لَيَّۢا بِأَلۡسِنَتِهِمۡ وَطَعۡنٗا فِي ٱلدِّينِۚ وَلَوۡ أَنَّهُمۡ قَالُواْ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَا وَٱسۡمَعۡ وَٱنظُرۡنَا لَكَانَ خَيۡرٗا لَّهُمۡ وَأَقۡوَمَ وَلَٰكِن لَّعَنَهُمُ ٱللَّهُ بِكُفۡرِهِمۡ فَلَا يُؤۡمِنُونَ إِلَّا قَلِيلٗا

Miongoni mwa Mayahudi wamo wanaopotosha maneno kuyatoa pahali pake, na husema: Tumesikia na tumeasi, na sikia bila ya kusikizishwa. Na husema: "Raai'naa", kwa kuzipotoa ndimi zao na kuitukana Dini. Na lau kama wangelisema: Tumesikia na tumetii, na usikie na "Undhurna (Utuangalie)," ingelikuwa heri kwao na ya unyoofu zaidi. Lakini Mwenyezi Mungu aliwalaani kwa kufuru yao; basi hawaamini isipokuwa wachache tu. info
التفاسير:

external-link copy
47 : 4

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ ءَامِنُواْ بِمَا نَزَّلۡنَا مُصَدِّقٗا لِّمَا مَعَكُم مِّن قَبۡلِ أَن نَّطۡمِسَ وُجُوهٗا فَنَرُدَّهَا عَلَىٰٓ أَدۡبَارِهَآ أَوۡ نَلۡعَنَهُمۡ كَمَا لَعَنَّآ أَصۡحَٰبَ ٱلسَّبۡتِۚ وَكَانَ أَمۡرُ ٱللَّهِ مَفۡعُولًا

Enyi mliopewa Kitabu! Aminini tuliyoyateremsha yenye kusadikisha yale mliyo nayo, kabla hatujazifutilia mbali nyuso na kuzipeleka nyuma yake, au tuwalaani kama tulivyowalaani watu wa Sabato (Jumamosi). Na amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima ifanyike. info
التفاسير:

external-link copy
48 : 4

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغۡفِرُ أَن يُشۡرَكَ بِهِۦ وَيَغۡفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُۚ وَمَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱفۡتَرَىٰٓ إِثۡمًا عَظِيمًا

Hakika, Mwenyezi Mungu hafuti dhambi ya kushirikishwa, na hufuta dhambi ya yale yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, basi hakika amezua dhambi kubwa. info
التفاسير:

external-link copy
49 : 4

أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يُزَكُّونَ أَنفُسَهُمۚ بَلِ ٱللَّهُ يُزَكِّي مَن يَشَآءُ وَلَا يُظۡلَمُونَ فَتِيلًا

Je, hukuwaona wale wanaojitakasa nafsi zao? Bali Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye. Na hawatadhulumiwa hata kiasi cha kijiuzi kilichomo ndani ya uwazi wa kokwa ya tende. info
التفاسير:

external-link copy
50 : 4

ٱنظُرۡ كَيۡفَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَۖ وَكَفَىٰ بِهِۦٓ إِثۡمٗا مُّبِينًا

Tazama namna wanavyomzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na haya yanatosha kuwa dhambi iliyo wazi. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 4

أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ أُوتُواْ نَصِيبٗا مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡجِبۡتِ وَٱلطَّٰغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ هَٰٓؤُلَآءِ أَهۡدَىٰ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ سَبِيلًا

Je, hukuwaona wale waliopewa fungu katika Kitabu? Wanaamini masanamu na Taghut! Na wanasema kuhusu wale waliokufuru kwamba hawa ndio walioongoka zaidi katika njia kuliko wale walioamini. info
التفاسير: