ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
19 : 14

أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۚ إِن يَشَأۡ يُذۡهِبۡكُمۡ وَيَأۡتِ بِخَلۡقٖ جَدِيدٖ

Huoni kuwa Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa Haki? Akitaka atakuondoeni na alete viumbe wapya! info

Ewe unae semezwa! Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi zisimame juu ya Haki kwa mujibu wa hikima yake? Na Mwenye kuweza haya basi anaweza kukuteketezeni, enyi makafiri, na akitaka akaleta viumbe wengine badala yenu nyinyi, ambao watakubali kuwepo kwake, na kwamba Yeye ni Mmoja wa pekee.

التفاسير:

external-link copy
20 : 14

وَمَا ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ بِعَزِيزٖ

Na hilo kwa Mwenyezi Mungu si jambo gumu. info

Na kuondoa huko na kuleta si muhali wala si uzito kwa Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
21 : 14

وَبَرَزُواْ لِلَّهِ جَمِيعٗا فَقَالَ ٱلضُّعَفَٰٓؤُاْ لِلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُوٓاْ إِنَّا كُنَّا لَكُمۡ تَبَعٗا فَهَلۡ أَنتُم مُّغۡنُونَ عَنَّا مِنۡ عَذَابِ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖۚ قَالُواْ لَوۡ هَدَىٰنَا ٱللَّهُ لَهَدَيۡنَٰكُمۡۖ سَوَآءٌ عَلَيۡنَآ أَجَزِعۡنَآ أَمۡ صَبَرۡنَا مَا لَنَا مِن مَّحِيصٖ

Na wote watahudhuria mbele ya Mwenyezi Mungu. Wanyonge watawaambia walio takabari: Sisi tulikuwa wafwasi wenu; basi hebu hamtuondolei kidogo hivi katika adhabu ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Lau Mwenyezi Mungu angeli tuongoa basi hapana shaka nasi tungeli kuongoeni. Ni mamoja kwetu tukipapatika au tukisubiri; hatuna pa kukimbilia. info

Makafiri wote watadhihiri kutoka makaburini kwao, waonekane kwa ajili ya kuhisabiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kudhihiri huko hakuna shaka, ni kama kwamba yametokea hivi sasa. Hapo wale wenye maoni ya kinyonge miongoni mwa wafwasi watawaambia waongozi wenye kiburi: Sisi tulikuwa wafwasi wenu katika kuwakanusha Mitume na kuwapiga vita, na kuzipuuza nasaha zao. Basi je, hii leo, hamtuondolei kidogo baadhi ya adhabu? Wakubwa walio takabari watasema: Ingeli kuwa Mwenyezi Mungu ametuongoa kwenye njia ya kuokoka, na akatuwafikia, basi nasi tungeli kuongozeni na tungeli kuitieni muifuate hiyo njia. Walakini sisi tumepotea na kwa hivyo tukakupotezeni nyinyi, yaani tumekuchagulieni tuliyo jichagulia nafsi zetu. Na leo hii sisi na nyinyi ni sawa sawa, tukisikitika au tukastahamili. Hapana pa kuikimbilia adhabu hii!

التفاسير:

external-link copy
22 : 14

وَقَالَ ٱلشَّيۡطَٰنُ لَمَّا قُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ إِنَّ ٱللَّهَ وَعَدَكُمۡ وَعۡدَ ٱلۡحَقِّ وَوَعَدتُّكُمۡ فَأَخۡلَفۡتُكُمۡۖ وَمَا كَانَ لِيَ عَلَيۡكُم مِّن سُلۡطَٰنٍ إِلَّآ أَن دَعَوۡتُكُمۡ فَٱسۡتَجَبۡتُمۡ لِيۖ فَلَا تَلُومُونِي وَلُومُوٓاْ أَنفُسَكُمۖ مَّآ أَنَا۠ بِمُصۡرِخِكُمۡ وَمَآ أَنتُم بِمُصۡرِخِيَّ إِنِّي كَفَرۡتُ بِمَآ أَشۡرَكۡتُمُونِ مِن قَبۡلُۗ إِنَّ ٱلظَّٰلِمِينَ لَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Na Shet'ani atasema itapo katwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli. Nami nalikuahidini; lakini sikukutimizieni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu, isipo kuwa nilikuiteni, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu, wala nyinyi hamwezi kuwa watetezi wangu. Hakika mimi nilikataa tangu zamani kunishirikisha na Mwenyezi Mungu. Hakika madhaalimu watakuwa na adhabu chungu. info

Mwenyezi Mungu atapo pitisha amri yake, ya kuwaneemesha watii'fu, na kuwa adhibu wenye kuasi, Iblisi atawambia wanao mfuata, Hakika Mwenyzi Mungu amekuahidini ahadi ya kweli, kuhusu kufufuliwa na malipo, na ametimiza. Na mimi nimekuahidini ahadi ya uwongo ya kwamba hakuna kufufuliwa wala malipo, na mi mimwekenda kinyume na ahadi yangu. Nami sikuwa na nguvu juu yenu hata nikulazimishieni kunifuata lakini nimekuitieni kwa ushawishi wangu wa upotovu nanyi mukaja mbio kunitii, basi musinilaumu kwa sababu ya ushawishi wangu, na zilaumuni nasfi zenu kwa kuniitikia. Wala mimi hii leo siwakukuokoweni na adhabu, na nyinyi hamuwezi kunioa mimi. Mimi leo nakataa huko kunishirikisha mimi na Mwenyezi mugnu huko duniani mulipokuwa mukinit'ii, kama mtumwa anavyo mti'ii bwana wake. Hakika makafiri watapata adhabu chungu.

التفاسير:

external-link copy
23 : 14

وَأُدۡخِلَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا بِإِذۡنِ رَبِّهِمۡۖ تَحِيَّتُهُمۡ فِيهَا سَلَٰمٌ

Na walio amini na wakatenda mema wataingizwa katika Mabustani yapitayo mito kati yake, wadumu humo kwa idhini ya Mola wao Mlezi. Maamkio yao humo yatakuwa: Salaam. info

Na Akhera wataingizwa wenye kuamini, na wakatenda vitendo vyema, katika Mabustani yanayo pitiwa na mito chini ya majumba yake, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na amri yake. Maamkio yao humo kutokana na Malaika ni kufahamisha amani na utulivu.

التفاسير:

external-link copy
24 : 14

أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا كَلِمَةٗ طَيِّبَةٗ كَشَجَرَةٖ طَيِّبَةٍ أَصۡلُهَا ثَابِتٞ وَفَرۡعُهَا فِي ٱلسَّمَآءِ

Hebu hukuona vipi Mwenyezi Mungu alivyo piga mfano wa neno zuri? Ni kama mti mzuri, mizizi yake ni imara, na matawi yake yako mbinguni. info

Je, ewe mtu! Hujui vipi Mwenyezi Mungu alivyo fananisha neno la Haki lilio zuri, na neno la uwongo lilio baya? Amelimathili neno zuri lenye faida kuwa ni kama mti wenye manufaa. Asili yake ni mizizi iliyo shikilia baraabara kwenye ardhi na matawi yake yamenyanyuka kuelekea mbinguni.

التفاسير: