ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
35 : 16

وَقَالَ ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ لَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا عَبَدۡنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَيۡءٖ نَّحۡنُ وَلَآ ءَابَآؤُنَا وَلَا حَرَّمۡنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَيۡءٖۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ فَهَلۡ عَلَى ٱلرُّسُلِ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ

Na washirikina walisema, «Lau kama Mwenyezi Mungu Alitaka tumuabudu Yeye Peke Yake, hatungalimuabudu yoyote asiyekuwa Yeye, sisi wala baba zetu kabla yetu, wala hatungaliharamisha chochote Asichokiharamisha». Ni hoja kama hizi za kipotofu walizozitumia makafifiri waliopita. Na wao ni warongo, kwani Mwenyezi Mungu Aliwaamrisha na Akawakataza na Akawawezesha kuyasimamia Aliyowakalifisha nayo, na Akawapa nguvu na matakwa yanayotokamana na vitendo vyao. Kwa hivyo, kujenga hoja kwao wakitegemea mapitisho ya Mwenyezi Mungu na makadirio Yake ni ubatilifu mkubwa baada ya kuonywa kwao na Mitume. Na Mitume wenye kuwaonya hawana la zaidi isipokuwa kuufikisha ujumbe ulio wazi waliokalifishwa nao. info
التفاسير:

external-link copy
36 : 16

وَلَقَدۡ بَعَثۡنَا فِي كُلِّ أُمَّةٖ رَّسُولًا أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَٱجۡتَنِبُواْ ٱلطَّٰغُوتَۖ فَمِنۡهُم مَّنۡ هَدَى ٱللَّهُ وَمِنۡهُم مَّنۡ حَقَّتۡ عَلَيۡهِ ٱلضَّلَٰلَةُۚ فَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَٱنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُكَذِّبِينَ

Kwa hakika tulipeleka kwa kila ummah uliopita mjumbe wa kuwaamrisha wao kumuabudu Mwenyezi Mungu na kumtii Peke Yake, na kuacha kumuabudu asiyekuwa Yeye miongoni mwa Mashetani, mizimu, wafu na vinginevyo kati ya vile vinavyotegemewa badala ya Mwenyezi Mungu. Basi wakawa miongoni mwao wale ambao Mwenyezi Mungu aliwaongoa wakafuata njia ya Mitume, na kati yao wakapatikana wakaidi waliofuata njia za upotofu, hapo ikapasa kwao upotevu na Mwenyezi Mungu Asiwaafikie. Basi tembeeni katika ardhi na mjionee kwa macho yenu vipi yalivyokuwa marejeo ya hawa wakanushaji na maangamivu yaliyowashukia, mpate kuzingatia? info
التفاسير:

external-link copy
37 : 16

إِن تَحۡرِصۡ عَلَىٰ هُدَىٰهُمۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي مَن يُضِلُّۖ وَمَا لَهُم مِّن نَّٰصِرِينَ

Utakapofanya bidii yako ya mwisho, ewe Mtume, kuwaongoa hawa washirikina, basi jua kwamba Mwenyezi Mungu Hamuongozi Anayepotosha, na hawana wao yoyote asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayewaokoa na kuwazuilia adhabu Yake. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 16

وَأَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ لَا يَبۡعَثُ ٱللَّهُ مَن يَمُوتُۚ بَلَىٰ وَعۡدًا عَلَيۡهِ حَقّٗا وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ

Na hawa washirikina waliapa kwa Mwenyezi Mungu viapo vizito kwamba Mwenyezi Mungu Hatamfufua aliyekufa baada na kumalizika na kutawanyika. Kwani, Atawafufufa Mwenyezi Mungu kwa lazima, hiyo ni ahadi ya kweli Aliyojilazimisha nayo, lakini wengi wa watu hawaujui uweza wa Mwenyezi Mungu wa kufufua, ndio maana wanaukanusha. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 16

لِيُبَيِّنَ لَهُمُ ٱلَّذِي يَخۡتَلِفُونَ فِيهِ وَلِيَعۡلَمَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّهُمۡ كَانُواْ كَٰذِبِينَ

Mwenyezi Mungu Atwafufua waja wote, ili awafunulie ukweli wa Ufufuzi ambao wametafautiana juu yake, na ili makafiri wenye kuukanusha wapate kujua kwamba wao wako kwenye ubatilifu na kwamba wao ni warongo pindi walipoapa kwamba hakuna kufufuliwa. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 16

إِنَّمَا قَوۡلُنَا لِشَيۡءٍ إِذَآ أَرَدۡنَٰهُ أَن نَّقُولَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ

Hakika jambo la kufufua ni pesi kwetu. Kwani sisi tutakapo kitu, tunakiambia «Kuwa» ukitahamaki kimeshakuwa na kimeshapatikana. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 16

وَٱلَّذِينَ هَاجَرُواْ فِي ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا ظُلِمُواْ لَنُبَوِّئَنَّهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗۖ وَلَأَجۡرُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ

Na wale walioacha makao yao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na wakahama baada ya matukio ya kudhulumiwa, tutawakalisha duniani makao mema. Na malipo ya Akhera ni makubwa zaidi, kwani malipo yao huko ni Pepo. Lau wale waliosalia nyuma wakaacha kugura wanayajuwa, ujuzi wa uhakika, yale yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ya malipo na thawabu kwa wale wanaogura katika njia Yake, hangalisalia nyuma yoyote katika wao. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 16

ٱلَّذِينَ صَبَرُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ

Hawa wenye kugura katika njia ya Mwenyezi Mungu ndio waliovumilia juu ya amri ya Mwenyezi Mungu na makatazo Yake na juu ya makadirio Yake yenye uchungu, na kwa Mola wao Peke Yake wanategemea, ndipo wakastahiki cheo hiki kikubwa. info
التفاسير: