ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
15 : 16

وَأَلۡقَىٰ فِي ٱلۡأَرۡضِ رَوَٰسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمۡ وَأَنۡهَٰرٗا وَسُبُلٗا لَّعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ

Na Ameyakitisha kwenye ardhi majabali ya kuithibitisha ili isije ikawayumbisha nyinyi, na Ameiweka humo mito ili mpate kunywa maji yake, na Amefanya humo njia nyingi ili mpate kuongoka kwa njia hizo kuzifikia sehemu mnazozikusudia. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 16

وَعَلَٰمَٰتٖۚ وَبِٱلنَّجۡمِ هُمۡ يَهۡتَدُونَ

Na kwenye hiyo ardhi Ameweka alama ambazo kwa alama hizo mnajielekeza njia kipindi cha mchana, kama alivyoziweka nyota ili kujiongoza kwa nyota hizo kipindi cha usiku. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 16

أَفَمَن يَخۡلُقُ كَمَن لَّا يَخۡلُقُۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ

Basi mnamfanya Mwenyezi Mungu Ambaye Anaviumba vitu hivyi na vinginevyo, katika kustahiki Kwake kuabudiwa Peke Yake, ni kama waungu wanaodaiwa ambao hawaumbi chochote? Basi hamukumbuki utukufu wa Mwenyezi Mungu mkamuabudu Yeye Peke Yake? info
التفاسير:

external-link copy
18 : 16

وَإِن تَعُدُّواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ لَا تُحۡصُوهَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na mkijaribu kuzidhibiti neema za Mwenyezi Mungu kwenu, ili mjue idadi yake, hamuwezi kuzidhibiti kwa wingi wake na utafauti wake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, ni Mwenye huruma kwenu, kwani Anasamehe kasoro zenu za kutotekeleza ushukuru wa neema, wala Hazikati kwenu, kwa kukiuka kwenu mipaka, wala Hawaharakishii mateso. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 16

وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعۡلِنُونَ

Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakata na kila aina ya upungufu, Anayajua matendo yenu yote, sawasawa yale mnayoyaficha ndani ya nafsi zenu kati ya hayo na yale mnayoyafanya waziwazi mbele ya wengine, na Atawalipa kwayo. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 16

وَٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَا يَخۡلُقُونَ شَيۡـٔٗا وَهُمۡ يُخۡلَقُونَ

Na wale waungu ambao washirikina wanawaabudu hawaumbi chochote hata kama ni kidogo vipi. Hao ni viumbe ambazo washirikina wamevitengeneza kwa mikono yao. Vipi basi wataviabudu? info
التفاسير:

external-link copy
21 : 16

أَمۡوَٰتٌ غَيۡرُ أَحۡيَآءٖۖ وَمَا يَشۡعُرُونَ أَيَّانَ يُبۡعَثُونَ

Wote hao ni visiki, havina uhai, wala hawajui wakati ambao Mwenyezi Mungu Atawafufua wale wanaowaabudu. Na waungu hao pamoja na wanaowaabudu wote watatupwa Motoni Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 16

إِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۚ فَٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ قُلُوبُهُم مُّنكِرَةٞ وَهُم مُّسۡتَكۡبِرُونَ

Mola wenu Ndiye Mstahiki wa kuabudiwa Peke Yake. Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Mmoja Peke Yake, hivyo basi wale wasioamini kufufuliwa, nyoyo zao ni zenye kuukanusha upweke Wake, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, kwa kutoogopa mateso Yake. Kwa hivyo, wao wana ujeuri wa kutoikubali haki na kukataa kumuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 16

لَا جَرَمَ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعۡلِنُونَۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡتَكۡبِرِينَ

Ni kweli kwamba Mwenyezi Mungu Anayajua wanayoyaficha ya itikadi, maneno na vitendo, na wanayoyaonyesha waziwazi katika hayo, na Atawalipa kwa hayo. Kwa kweli Yeye, Aliyeshinda na kutukuka, Hawapendi wanaofanya ujeuri wa kukataa kumuabudu na kumtii, na Atawalipa kwa hilo. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 16

وَإِذَا قِيلَ لَهُم مَّاذَآ أَنزَلَ رَبُّكُمۡ قَالُوٓاْ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ

Na pindi wanapoulizwa, hawa washirikina, kuhusu yale yaliyoteremshiwa Nabii Muhammad, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, wanasema kwa urongo na uzushi, «Hakuleta isipokuwa visa vya waliotangulia na porojo zao.» info
التفاسير:

external-link copy
25 : 16

لِيَحۡمِلُوٓاْ أَوۡزَارَهُمۡ كَامِلَةٗ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَمِنۡ أَوۡزَارِ ٱلَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيۡرِ عِلۡمٍۗ أَلَا سَآءَ مَا يَزِرُونَ

Mwisho wao utakuwa ni kuzibeba dhambi zao kamili Siku ya Kiyama, hawatasamehewa chochote, na watazibeba dhambi za wale waliowadanganya ili kuwaepusha na Uislamu, bila ya kupunguziwa dhambi zao. Jueni mtanabahi, ni ubaya ulioje wa dhambi watakazozibeba! info
التفاسير:

external-link copy
26 : 16

قَدۡ مَكَرَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ فَأَتَى ٱللَّهُ بُنۡيَٰنَهُم مِّنَ ٱلۡقَوَاعِدِ فَخَرَّ عَلَيۡهِمُ ٱلسَّقۡفُ مِن فَوۡقِهِمۡ وَأَتَىٰهُمُ ٱلۡعَذَابُ مِنۡ حَيۡثُ لَا يَشۡعُرُونَ

Kabla ya washirikina hawa, makafiri waliwafanyia vitimbi Mitume wao, na kuifanyia vitimbi haki waliokuja nayo. Hapo amri ya Mwenyezi Mungu ililijia jengo lao kutoka kwenye asili yake na msingi wake, na sakafu ikawaangukia, na maangamivu yakawajia kwenye sehemu ambazo walijimakini kuwa ni za amani, kutoka mahali wasipodhania kuwa maangamivu yatawajia kutoka hapo. info
التفاسير: