ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
53 : 12

۞ وَمَآ أُبَرِّئُ نَفۡسِيٓۚ إِنَّ ٱلنَّفۡسَ لَأَمَّارَةُۢ بِٱلسُّوٓءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّيٓۚ إِنَّ رَبِّي غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Akasema mke wa kiongozi,»Sijisafishi nafsi yangu, kwani nafsi inamwamrisha mtu sana kufanya maasia, kwa kutaka kupata utamu wa inavyopenda, isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu Amemhifadhi. Kwani Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe dhambi za waliotubia miongoni mwa waja Wake, ni Mwenye huruma nao sana.» info
التفاسير:

external-link copy
54 : 12

وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ ٱئۡتُونِي بِهِۦٓ أَسۡتَخۡلِصۡهُ لِنَفۡسِيۖ فَلَمَّا كَلَّمَهُۥ قَالَ إِنَّكَ ٱلۡيَوۡمَ لَدَيۡنَا مَكِينٌ أَمِينٞ

Mfalme, mtawala wa Misri, ilipomfikia habari kwamba Yūsuf hana hatia, alisema, «Mleteni kwangu nipate kumfanya ni miongoni mwa marafiki wangu wa kikweli na washauri wangu.» Yūsuf alipokuja, na mfalme akasema na yeye, akajua kwamba yeye hana hatia na kwamba ni muaminifu sana na ni mwenye tabia njema, alimwambia, «Wewe leo hapa kwetu una heshima kubwa na unaaminiwa kwa kila kitu.» info
التفاسير:

external-link copy
55 : 12

قَالَ ٱجۡعَلۡنِي عَلَىٰ خَزَآئِنِ ٱلۡأَرۡضِۖ إِنِّي حَفِيظٌ عَلِيمٞ

Yūsuf akataka kuwanufaisha waja na kueneza uadilifu baina yao, alimwambia mfalme, «Nifanye mimi kuwa msimamizi wa hazina za Misri, kwani mimi ni mshika hazina mwaminifu mwenye ujuzi na busara juu ya vitu ninavyosimamia.» info
التفاسير:

external-link copy
56 : 12

وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي ٱلۡأَرۡضِ يَتَبَوَّأُ مِنۡهَا حَيۡثُ يَشَآءُۚ نُصِيبُ بِرَحۡمَتِنَا مَن نَّشَآءُۖ وَلَا نُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na kama Mwenyezi Mungu Alivyomneemesha Yūsuf kwa kumtoa jela, Alimmakinisha katika nchi ya Misri akawa ashukia popote pale anapotaka. Mwenyezi Mungu Anampa rehema Zake Anayemtaka kati ya waja wake wachamungu, na Hayapotezi malipo ya yoyote aliyefanya matendo mema. info
التفاسير:

external-link copy
57 : 12

وَلَأَجۡرُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَكَانُواْ يَتَّقُونَ

Na kwa hakika malipo mema ya Akhera ni makubwa zaidi kuliko malipo ya duniani kwa wenye Imani na uchamungu ambao wanayaogopa mateso ya Mwenyezi Mungu na wanamtii Yeye katika maamrisho Yake na makatazo Yake. info
التفاسير:

external-link copy
58 : 12

وَجَآءَ إِخۡوَةُ يُوسُفَ فَدَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَعَرَفَهُمۡ وَهُمۡ لَهُۥ مُنكِرُونَ

Nduguze Yūsuf walifika Misri, baada ya kushukiwa na ukame katika nchi yao, ili wachukue chakula kutoka huko. Wakaingia kwake na yeye, kwa nguvu ya akili yake ya kutambua na werevu wake, akawajua na wao wasimjue kwa muda mrefu uliopita na kwa kubadilika umbo lake. info
التفاسير:

external-link copy
59 : 12

وَلَمَّا جَهَّزَهُم بِجَهَازِهِمۡ قَالَ ٱئۡتُونِي بِأَخٖ لَّكُم مِّنۡ أَبِيكُمۡۚ أَلَا تَرَوۡنَ أَنِّيٓ أُوفِي ٱلۡكَيۡلَ وَأَنَا۠ خَيۡرُ ٱلۡمُنزِلِينَ

Yūsuf aliamuru wakirimiwe na wakaribishwe vizuri, kisha akawapa chakula walichotaka. Na walikuwa wamemwambia kwamba wana ndugu yao wa kwa baba ambaye hawakumleta pamoja nao, wakimaanisha ndugu yake Binyamin, akasema, «Nileteeni ndugu yenu wa kwa baba, kwani hamuoni kwamba mimi nimewapimia chakula vizuri na nimewakirimu kwa kuwakaribisha, na mimi ni mwema wa kuwakaribisha? info
التفاسير:

external-link copy
60 : 12

فَإِن لَّمۡ تَأۡتُونِي بِهِۦ فَلَا كَيۡلَ لَكُمۡ عِندِي وَلَا تَقۡرَبُونِ

«Na msiponijia na yeye, basi nyinyi hamtakua na chakula ambacho mimi nitawapimia, na msije kwangu.» info
التفاسير:

external-link copy
61 : 12

قَالُواْ سَنُرَٰوِدُ عَنۡهُ أَبَاهُ وَإِنَّا لَفَٰعِلُونَ

Wakasema, «Tutafanya bidii yetu kumkinaisha baba yake atuachie, na hatutaacha kufanya hivyo.» info
التفاسير:

external-link copy
62 : 12

وَقَالَ لِفِتۡيَٰنِهِ ٱجۡعَلُواْ بِضَٰعَتَهُمۡ فِي رِحَالِهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَعۡرِفُونَهَآ إِذَا ٱنقَلَبُوٓاْ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ

Yūsuf aliwaambia watumishi wake, «Ichukueni thamani ya vitu vyao muiweke kwenye vyombo vyao kwa siri, kwa matarajio wapate kuiona watakapofika kwao na watambue vile sisi tulivyowakirimu ili wapate kurudi wakiwa na matumaini ya kupata vipewa vyetu.» info
التفاسير:

external-link copy
63 : 12

فَلَمَّا رَجَعُوٓاْ إِلَىٰٓ أَبِيهِمۡ قَالُواْ يَٰٓأَبَانَا مُنِعَ مِنَّا ٱلۡكَيۡلُ فَأَرۡسِلۡ مَعَنَآ أَخَانَا نَكۡتَلۡ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ

Waliporejea kwa baba yao walimsimulia yaliyokuwa ya ukarimu aliowafanyia huyo kiongozi, na wakasema, «Yeye hatatupatia kitu mbeleni isipokuwa iwapo ndugu yetu ambaye tulimuelezea kuhusu yeye atakuwa na sisi. Basi tuachie tuende na yeye tutaleta chakula kingi, na tunakuahidi kwamba tutamtunza.» info
التفاسير: