ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
104 : 12

وَمَا تَسۡـَٔلُهُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ

Na hutaki kwa watu wako ujira ya kuwaongoa kwenye Imani. Na yale uliyotumwa nayo ya Qur’ani na uongofu ni mawaidha kwa watu wote wanajikumbusha kwayo na wanaongoka. info
التفاسير:

external-link copy
105 : 12

وَكَأَيِّن مِّنۡ ءَايَةٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ يَمُرُّونَ عَلَيۡهَا وَهُمۡ عَنۡهَا مُعۡرِضُونَ

Na dalili zenye kuonyesha upweke wa Mwenyezi Mungu na uwezo Wake ni nyinygi, zimeenea kwenye mbingu na ardhi, kama jua, mwezi, majabali na miti. Wanaziona lakini wamezipa mgongo, hawazifikirii na wala hawazingatii. info
التفاسير:

external-link copy
106 : 12

وَمَا يُؤۡمِنُ أَكۡثَرُهُم بِٱللَّهِ إِلَّا وَهُم مُّشۡرِكُونَ

Na hawa wenye kuzipa mgongo dalili za Mwenyezi Mungu hawakubali kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaumba, ni Mwenye kuwapa riziki, ni Muumba wa kila kitu na ni Mstahiki wa kuabudiwa isipokuwa katika hali ya kumshirikisha kwa kuabudu kwao masanamu na mizimu. Mwenyezi Mungu Ametukuka na kuepukana na hilo kabisa. info
التفاسير:

external-link copy
107 : 12

أَفَأَمِنُوٓاْ أَن تَأۡتِيَهُمۡ غَٰشِيَةٞ مِّنۡ عَذَابِ ٱللَّهِ أَوۡ تَأۡتِيَهُمُ ٱلسَّاعَةُ بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ

Je, wana chochote kinachowafanya wameaminika isiwashukie wao adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu yenye kuwaenea au iwajie wao Siku ya Kiyama ghafla na hali wao hawatambui wala hawana hisia na hilo. info
التفاسير:

external-link copy
108 : 12

قُلۡ هَٰذِهِۦ سَبِيلِيٓ أَدۡعُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا۠ وَمَنِ ٱتَّبَعَنِيۖ وَسُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Waambie, ewe Mtume, «Hii ni njia yangu, ninaita kwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake, nikiwa kwenye hoja inayotoka kwa Mwenyezi Mungu na uhakika, mimi na anayenifuata. Na ninamuepusha Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, na washirika na mimi si katika wale wanaomshirikisha pamoja na Mwenyezi Mungu mtu mwingine.» info
التفاسير:

external-link copy
109 : 12

وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ إِلَّا رِجَالٗا نُّوحِيٓ إِلَيۡهِم مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡقُرَىٰٓۗ أَفَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۗ وَلَدَارُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Hatukuwatuma kabla yako, ewe Mtume, kwa watu isipokuwa wanaume miongoni mwao ambao tunawateremshia wahyi wetu, na wao ni miongoni mwa watu wa mijini, kwani hao wana uwezo zaidi wa kuuelewa ulinganizi na ujumbe, wawaamini wenye kuongoka kwenye haki na wawakanusha wenye kupotea njia yake. Basi si watembee katika ardhi wajionee ulikuwa vipi mwisho wa wakanushaji waliopita na ni maangamivu gani yaliyowashukia? Na malipo mema ya Nyumba ya Akhera ni bora kuliko dunia na vilivyomo ndani, kwa walioamini na wakamuogopa Mola wao. Basi hamfikirii mkazingatia? info
التفاسير:

external-link copy
110 : 12

حَتَّىٰٓ إِذَا ٱسۡتَيۡـَٔسَ ٱلرُّسُلُ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُمۡ قَدۡ كُذِبُواْ جَآءَهُمۡ نَصۡرُنَا فَنُجِّيَ مَن نَّشَآءُۖ وَلَا يُرَدُّ بَأۡسُنَا عَنِ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ

Na usiwe na haraka, ewe Mtume, ya kupata ushindi juu ya wanaokukanusha, kwani Mitume kabla yako hawakuwa wakijiwa na ushindi wa haraka kwa hekima tunayoijua. Ifikapo hadi ya Mitume kukata tamaa na watu wao na kuwa na hakika kwamba watu wao wamewakanusha na hakuna tamaa ya wao kuamini, ushindi utawajia wakati ambapo shida imezidi, basi hapo tuwaokoe tunaowataka kati ya Mitume na wafuasi wao. Na adhabu yetu haitorudishwa kutoka kwa Aliyefanya uhalifu na akmfanyia ujasiri Mwenyezi Mungu. Katika hili kuna kumliwaza Nabii, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. info
التفاسير:

external-link copy
111 : 12

لَقَدۡ كَانَ فِي قَصَصِهِمۡ عِبۡرَةٞ لِّأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِۗ مَا كَانَ حَدِيثٗا يُفۡتَرَىٰ وَلَٰكِن تَصۡدِيقَ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَتَفۡصِيلَ كُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ

Kwa hakika kwenye habari za Mitume tulizokuelezea na mambo yaliyowakumba wenye kukanusha kuna mawaidha kwa wenye akili timamu. Hii Qur’ani haikuwa ni habari ya urongo iliyozuliwa, lakini tumeiteremsha ikiwa ni yenye kutolea ushahidi ukweli wa vitabu vilivyoteremshwa vilivyotangulia na kwamba vinatoka kwa Mwenyezi Mungu, na ikiwa ni ufafanuzi wa kila ambalo waja wanalihitaji la kuhalalishiwa na kuharamishiwa, linalopendeza na linalochukiza na mengineyo, na ikiwa ni muelekezo kutoka kwenye upotevu na ni rehema, kwa wenye Imani, ya kuzifanya nyoyo zao ziongoke, wapate kuyafuata kivitendo maamrisho na makatazo yaliyomo. info
التفاسير: