Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Ali Muhsin Albirwany

Numero di pagina:close

external-link copy
60 : 28

وَمَآ أُوتِيتُم مِّن شَيۡءٖ فَمَتَٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَزِينَتُهَاۚ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰٓۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Na chochote mlicho pewa ni matumizi ya maisha ya dunia na pambo lake. Na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ndio bora na yatakayo baki zaidi. Basi je, hamfahamu? info

Na kila kitu mlicho ruzukiwa katika starehe za dunia na mapambo yake kina ukomo wake kwa muda mfupi. Hayo yasikuzuieni kuamini na kutenda vitendo vyema. Kwani hakika yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu huko Akhera, nayo ni thawabu na neema za milele, yana nafuu zaidi, na yana dawamu kuliko hayo yote. Basi kwa nini hamtumii akili zenu badala ya pumbao zenu?

التفاسير:

external-link copy
61 : 28

أَفَمَن وَعَدۡنَٰهُ وَعۡدًا حَسَنٗا فَهُوَ لَٰقِيهِ كَمَن مَّتَّعۡنَٰهُ مَتَٰعَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا ثُمَّ هُوَ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ مِنَ ٱلۡمُحۡضَرِينَ

Je! Yule tuliye muahidi ahadi nzuri, tena naye akayapata, ni kama tuliye mstarehesha kwa starehe za maisha ya duniani, na kisha Siku ya Kiyama akawa miongoni mwa wanao hudhurishwa? info

Hawi sawa mwenye kuamini na akatenda mema na akastahiki ahadi ya Mwenyezi Mungu na ahadi ya malipo mema na Pepo, na akayapata kama alivyo muahidi Mwenyezi Mungu; kulingana huyu na yule aliye kanusha na akatenda vitendo viovu, na yakamzuga maisha ya dunia na mapambo yake, na kisha Siku ya Kiyama akawa katika walio hudhurishwa kwa ajili ya hisabu, na akawa katika wenye kuhiliki kwa adhabu.

التفاسير:

external-link copy
62 : 28

وَيَوۡمَ يُنَادِيهِمۡ فَيَقُولُ أَيۡنَ شُرَكَآءِيَ ٱلَّذِينَ كُنتُمۡ تَزۡعُمُونَ

Na siku atakapo waita na akasema: Wako wapi mlio kuwa mkidai kuwa ni washirika wangu? info

Ewe Mtume! Kumbuka siku watapo simama hawa mbele ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuhisabiwa, naye Subhanahu akawaita kwa kuwatahayarisha: Wako wapi hao miungu mlio dai kuwa ni washirika wangu, wapate kukuteteeni na kukuombeeni?

التفاسير:

external-link copy
63 : 28

قَالَ ٱلَّذِينَ حَقَّ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقَوۡلُ رَبَّنَا هَٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ أَغۡوَيۡنَآ أَغۡوَيۡنَٰهُمۡ كَمَا غَوَيۡنَاۖ تَبَرَّأۡنَآ إِلَيۡكَۖ مَا كَانُوٓاْ إِيَّانَا يَعۡبُدُونَ

Watasema wale iliyo thibiti juu yao kauli: Mola wetu Mlezi! Hawa ndio tulio wapoteza. Tuliwapoteza kama tulivyo potea sisi. Tunajitenga nao mbele yako. Hawakuwa wakituabudu sisi. info

Watasema waongozi wa makafiri katika walio stahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na vitisho vyake: Ewe Mola wetu Mlezi! Hawa tulio waita kwenye shirki na tukawapambia upotovu tuliwapoteza. Kwa sababu wao walikhiari ukafiri na wakaupokea, kama sisi tulivyo ukhiari na tukaupokea. Leo sisi tunajitenga nao kwako na ukafiri walio ukhiari duniani. Hawakuwa wao wakituabudu sisi; bali wakiabudu pumbao zao, na wakit'ii matamanio yao.

التفاسير:

external-link copy
64 : 28

وَقِيلَ ٱدۡعُواْ شُرَكَآءَكُمۡ فَدَعَوۡهُمۡ فَلَمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَهُمۡ وَرَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَۚ لَوۡ أَنَّهُمۡ كَانُواْ يَهۡتَدُونَ

Na itasemwa: Waiteni hao miungu wa kishirikina wenu! Basi watawaita, lakini hawatawaitikia, na wataiona adhabu; laiti wangeli kuwa wameongoka! info

Na Mwenyezi Mungu kuwaamrisha makafiri ni kwa kuwatahayarisha tu, kwa vile kuwataka wawaite wale miungu ya ushirikina wawaokoe na adhabu yake, kama walivyo dai. Wakaitikia kwa unyonge, na wakawaita kwa kuwa hawana hila. Wasipate jawabu yoyote. Wakaiona adhabu walio ahidiwa iko mbele yao, na wakatamani lau kuwa katika dunia yao wangeli kuwa Waumini walio ongoka, jinsi ya adhabu iliyo wafikia.

التفاسير:

external-link copy
65 : 28

وَيَوۡمَ يُنَادِيهِمۡ فَيَقُولُ مَاذَآ أَجَبۡتُمُ ٱلۡمُرۡسَلِينَ

Na siku atapo waita na akasema: Mliwajibu nini Mitume? info

Na ewe Mtume! Taja vile vile siku washirikina watapo itwa na Mwenyezi Mungu kwa kutahayarishwa, na wakaambiwa: Mliwajibu nini Mitume wangu nilio watuma kwenu wakuiteni kwenye Imani, nao wakafikisha Ujumbe?

التفاسير:

external-link copy
66 : 28

فَعَمِيَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلۡأَنۢبَآءُ يَوۡمَئِذٖ فَهُمۡ لَا يَتَسَآءَلُونَ

Basi zitawapotea khabari siku hiyo, nao hawataulizana. info

Khabari hizo zikawapita hawazitambui kama kwamba ni vipofu. Ikawa hapana amuulizae mwenziwe, kwani wote walikuwa sawa sawa wameshindwa kujibu.

التفاسير:

external-link copy
67 : 28

فَأَمَّا مَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَعَسَىٰٓ أَن يَكُونَ مِنَ ٱلۡمُفۡلِحِينَ

Ama mwenye kutubu na akaamini na akatenda mema, huyo atakuwa miongoni mwa wenye kufanikiwa. info

Hii ndiyo hali ya washirikina. Ama mwenye kutubu kutokana na shirki yake, na akaamini Imani ya kweli, na akatenda mema, basi huyo hutaraji kuwa kwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa walio fuzu kuipata radhi ya Mwenyezi Mungu, na neema ya kudumu yenye kuendelea milele.

التفاسير:

external-link copy
68 : 28

وَرَبُّكَ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُ وَيَخۡتَارُۗ مَا كَانَ لَهُمُ ٱلۡخِيَرَةُۚ سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Na Mola wako Mlezi huumba na huteuwa atakavyo. Viumbe hawana khiari. Mwenyezi Mungu ametukuka na ametakasika na hao wanao washirikisha naye. info

Na Mola wako Mlezi anaumba atakalo kwa uwezo wake. Na anamkhitari amtakaye kwa hikima yake kumpa Ujumbe na ut'iifu kwa kujua kwake mwenyewe kufaa kwao. Wala hawawezi viumbe, na wala si haki, kumchagulia Mwenyezi Mungu walitakalo katika dini potovu, na miungu ya uwongo. Mtukufu ametakasika shani yake na washirika.

التفاسير:

external-link copy
69 : 28

وَرَبُّكَ يَعۡلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمۡ وَمَا يُعۡلِنُونَ

Na Mola wako Mlezi anayajua yaliyo ficha vifua vyao, na wanayo yatangaza. info

Ewe Mtume! Mola wako Mlezi anajua baraabara yaliomo katika vifua vya washirikina ya uadui wao juu yako, na wanayo tangaza kwa ndimi zao ya kukushutumu na kukupinga kwa ulivyo teuliwa kupewa Utume.

التفاسير:

external-link copy
70 : 28

وَهُوَ ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ لَهُ ٱلۡحَمۡدُ فِي ٱلۡأُولَىٰ وَٱلۡأٓخِرَةِۖ وَلَهُ ٱلۡحُكۡمُ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ

Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye. Sifa zote njema ni zake Yeye, mwanzo na mwisho. Na hukumu ni yake Yeye. Na kwake Yeye mtarejeshwa. info

Na Mola wako Mlezi, ewe Mtume, ndiye Mwenyezi Mungu wa Haki, ndiye pekee Mwenye Ungu, Mwenye kustahiki peke yake kuhimidiwa na waja wake katika dunia kwa neema zake na uwongofu wake, na katika Akhera kwa uadilifu wake na kulipa kwake. Na Yeye peke yake ndiye Mwenye hukumu, na kuamua baina ya waja wake. Na kwake Yeye ndiyo marejeo ya kwendea.

التفاسير: