Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassara da harshen Sawahili - Abdullah Muhammad da Nasir Khamis

Lambar shafi: 474:467 close

external-link copy
67 : 40

هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَكُم مِّن تُرَابٖ ثُمَّ مِن نُّطۡفَةٖ ثُمَّ مِنۡ عَلَقَةٖ ثُمَّ يُخۡرِجُكُمۡ طِفۡلٗا ثُمَّ لِتَبۡلُغُوٓاْ أَشُدَّكُمۡ ثُمَّ لِتَكُونُواْ شُيُوخٗاۚ وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّىٰ مِن قَبۡلُۖ وَلِتَبۡلُغُوٓاْ أَجَلٗا مُّسَمّٗى وَلَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ

Yeye Ndiye Aliyemuumba baba yenu Ādam kwa mchanga, kisha Akawafanya mpatikane kutokana na manii kwa uweza Wake, na baada yake mnahamia kwenye mwongo wa damu nzito iliyo nyekundu, kisha mnapitiwa na miongo kadha ndani ya vizazi, mpaka mnapozaliwa mkiwa watoto wadogo, kisha umbile lenu linapata nguvu (na mnaendelea hivyo) mpaka mnapokuwa wazee, na miongoni mwenu kuna wanaokufa kabla ya hapo. Na ili mfikie kwa miongo hii kipindi kiliotajwa ambacho hapo umri wenu ukome. Huenda nyinyi mkazitia akilini hoja za Mwenyezi Mungu katika hilo na mkazizingatia aya zake mkajua kuwa hakuna Mola isipokuwa Yeye Anayefanya hilo, na kwamba Yeye Ndiye Ambaye haitakiwi kuabudiwa isipokuwa Yeye. info
التفاسير:

external-link copy
68 : 40

هُوَ ٱلَّذِي يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ فَإِذَا قَضَىٰٓ أَمۡرٗا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ

Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Aliyepwekeka kwa kuhuisha na kufisha. Na Akiamua jambo Analiambia, «Kuwa!» na likawa, hakuna mwenye kurudisha uamuzi Wake. info
التفاسير:

external-link copy
69 : 40

أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يُجَٰدِلُونَ فِيٓ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ أَنَّىٰ يُصۡرَفُونَ

Je, huwaonei ajabu, ewe Mtume, hawa wakanushaji wa aya za Mwenyezi Mungu vile wanavyoshindana nazo, na hali hizo ziko wazi katika kutolea ushahidi upweke wa Mwenyezi Mungu na uweza Wake, ni vipi wao wanaziepuka pamoja na usahihi wake? Na wataenda kwenye kitu gani baada ya huu ufafanuzi kamili? info
التفاسير:

external-link copy
70 : 40

ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِٱلۡكِتَٰبِ وَبِمَآ أَرۡسَلۡنَا بِهِۦ رُسُلَنَاۖ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ

Washirikina hawa waliokanusha Qur’ani na Vitabu vya mbinguni Alivyoviteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mitume Wake ili kuongoza watu, watajua wakanushaji hawa mwisho wa ukanushaji wao. info
التفاسير:

external-link copy
71 : 40

إِذِ ٱلۡأَغۡلَٰلُ فِيٓ أَعۡنَٰقِهِمۡ وَٱلسَّلَٰسِلُ يُسۡحَبُونَ

Pindi watakapotiwa pingu kwenye shingo zao na minyonyoro kwenye miguu yao, na huku Malaika wa adhabu wakiwaburuta. info
التفاسير:

external-link copy
72 : 40

فِي ٱلۡحَمِيمِ ثُمَّ فِي ٱلنَّارِ يُسۡجَرُونَ

Wakiwatia kwenye maji moto yaliyochemka sana na yenye uharara mwingi, kisha wachomwe ndani ya Moto wa Jahanamu. info
التفاسير:

external-link copy
73 : 40

ثُمَّ قِيلَ لَهُمۡ أَيۡنَ مَا كُنتُمۡ تُشۡرِكُونَ

Kisha waambiwe kwa kuwasimanga, na wao wako kwenye hali hii ya unguliko , «Wako wapi waungu mliokuwa mkiwaabudu. info
التفاسير:

external-link copy
74 : 40

مِن دُونِ ٱللَّهِۖ قَالُواْ ضَلُّواْ عَنَّا بَل لَّمۡ نَكُن نَّدۡعُواْ مِن قَبۡلُ شَيۡـٔٗاۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ ٱلۡكَٰفِرِينَ

badala ya Mwenyezi Mungu? Je watawatetea nyinyi leo? Basi waiteni ili wawaokoe na balaa hii iliyowashukia iwapo wataweza.» Hapo wakanushaji waseme, «Wametupotea machoni hatuwaoni, na hawakutunufaisha kitu chochote.» Hapo wakubali kuwa wao walikuwa ujingani katika mambo yao, na kuwa kule kuabudu kwao wale waungu kulikuwa ni ubatilifu usio na faida yoyote. Na kama vile Mwenyezi Mungu Alivyowapoteza hawa waliowapotea katika moto wa Jahanamu waliokuwa wakiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, ndivyo Mwenyezi Mungu Anavyowapoteza wale wenye kumkanusha. info
التفاسير:

external-link copy
75 : 40

ذَٰلِكُم بِمَا كُنتُمۡ تَفۡرَحُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّ وَبِمَا كُنتُمۡ تَمۡرَحُونَ

Adhabu hiyo itakayowapata ni kwa sababu ya kughafilika mliokuwa nako katika uhai wenu wa kilimwengu, kwa kuwa mlikuwa mkifurahika na yale mnayoyatenda ya maasia na madhambi na tabia mliokuwa nazo za gogi, kiburi na kuwafanyia udhalimu waja wa Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
76 : 40

ٱدۡخُلُوٓاْ أَبۡوَٰبَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَاۖ فَبِئۡسَ مَثۡوَى ٱلۡمُتَكَبِّرِينَ

Ingieni kwenye milango ya Jahanamu ikiwa ni mateso yenu kwa kumkanusha kwenu Mwenyezi Mungu na kumuasi, hali ya kukaa milele humo. Ni mbaya sana Jahanamu kuwa ni mashukio ya wenye kumfanyia kuburi Mwenyezi Mungu duniani. info
التفاسير:

external-link copy
77 : 40

فَٱصۡبِرۡ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞۚ فَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعۡضَ ٱلَّذِي نَعِدُهُمۡ أَوۡ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيۡنَا يُرۡجَعُونَ

Basi vumilia, ewe Mtume, na uendelee katika njia ya ulinganizi, hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli na Atakutekelezea kile Alichokuahidi. Basi, ima tukuoneshe katika uhai wako sehemu ya adhabu tunayowaahidi hawa washirikina au tukufishe kabla ya hiyo adhabu kuwashukia, kwani ni kwetu sisi mwisho wao Siku ya Kiyama, na tutawaonjesha adhabu kali kwa yale waliokuwa wakiyakanusha. info
التفاسير: