Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - Fassara da harshen Sawahili - Abdullah Muhammad da Nasir Khamis

Lambar shafi: 475:467 close

external-link copy
78 : 40

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا رُسُلٗا مِّن قَبۡلِكَ مِنۡهُم مَّن قَصَصۡنَا عَلَيۡكَ وَمِنۡهُم مَّن لَّمۡ نَقۡصُصۡ عَلَيۡكَۗ وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأۡتِيَ بِـَٔايَةٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ فَإِذَا جَآءَ أَمۡرُ ٱللَّهِ قُضِيَ بِٱلۡحَقِّ وَخَسِرَ هُنَالِكَ ٱلۡمُبۡطِلُونَ

Hakika tuliwatumiliza kabla yako, ewe Mtume, Mitume wengi kwa watu wao wawalinganie na wavumilie udhia wao. Miongoni mwao kuna wale tuliokuhadithia habari zao, na miongoni mwao kuna wale ambao hatukukuhadithia. Na wote hao wameaminiwa kufikisha wahyi wa Mwenyezi Mungu kwa watu wao. Na haikuwa ni yenye kuwezekana kwa yoyote miongoni mwao kuleta alama yoyote miongoni mwa alama zinazoonekana au zinazofahamika isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na matakwa Yake. Basi itakapokuja amri ya Mwenyezi Mungu ya kuadhibiwa wakanushaji, itatolewa hukumu ya uadilifu baina ya Mitume na wale waliowakanusha, na hapo watapata hasara waliokuwa wabatilifu kwa kule kumzulia kwao Mwenyezi Mungu urongo na kuabudu kwao asiyekuwa Yeye. info
التفاسير:

external-link copy
79 : 40

ٱللَّهُ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَنۡعَٰمَ لِتَرۡكَبُواْ مِنۡهَا وَمِنۡهَا تَأۡكُلُونَ

Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, Ndiye Aliyewapa nyinyi wanyama , ili mnufaike nao kwa kupanda na kula info
التفاسير:

external-link copy
80 : 40

وَلَكُمۡ فِيهَا مَنَٰفِعُ وَلِتَبۡلُغُواْ عَلَيۡهَا حَاجَةٗ فِي صُدُورِكُمۡ وَعَلَيۡهَا وَعَلَى ٱلۡفُلۡكِ تُحۡمَلُونَ

na manufaa mengineyo, na ili mfikie, kwa kuwabebesha wengineo, haja ya nafsi zenu ya kufika miji ya mbali. Na juu ya wanyama hao mnabebwa barani, na juu ya majahazi mkiwa baharini mnabebwa pia. info
التفاسير:

external-link copy
81 : 40

وَيُرِيكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ فَأَيَّ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ تُنكِرُونَ

Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anawaonyesha dalili zake nyinygi zilizo wazi zenye kutolea ushahidi uweza Wake na uendeshaji mambo Wake. Basi ni dalili gani miongoni mwa dalili za Mwenyezi Mungu mnazikanusha na hamzikubali? info
التفاسير:

external-link copy
82 : 40

أَفَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَانُوٓاْ أَكۡثَرَ مِنۡهُمۡ وَأَشَدَّ قُوَّةٗ وَءَاثَارٗا فِي ٱلۡأَرۡضِ فَمَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ

Kwani hawakutembea kwenye ardhi wakanushaji hawa wakafikiria juu ya maangamivu ya ummah waliokanusha waliokuwa kabla yao ulikuwa vipi mwisho wao? Ummah hao waliopita walikuwa ni wengi kuliko wao kwa idadi, zana na athari ya majengo, viwanda, ukulima na yasiyokuwa hayo. Na yote hayo waliyoyatenda hayakuwafalia kitu ilipowateremkia wao adhabu ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
83 : 40

فَلَمَّا جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَرِحُواْ بِمَا عِندَهُم مِّنَ ٱلۡعِلۡمِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ

Walipowajia, hao ummah waliowakanusha, Mitume wao kwa dalili zilizo wazi, walifurahia, kwa ujinga wao, ujuzi walionao unaogongana na yale waliyokuja nayo Mitume, na ikawashukia wao ile adhabu waliokuwa wakiiharakisha kwa njia ya shere na dhihaka. Katika aya hii kuna dalili kuwa kila ujuzi unaogongana na Uislamu au kuutia kombo au kutilia shaka usahihi wake, basi ujuzi huo ni mwenye kutukanika na kuchukiza, na mwenye kuuamini si miongoni mwa wafuasi wa Muhammad, reheme ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. info
التفاسير:

external-link copy
84 : 40

فَلَمَّا رَأَوۡاْ بَأۡسَنَا قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَحۡدَهُۥ وَكَفَرۡنَا بِمَا كُنَّا بِهِۦ مُشۡرِكِينَ

Walipoiona adhabu yetu, walikubali wakati ambapo kukubali hakunufaishi, na wakasema, «Tumemuamini Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na tumekikanusha kile ambacho tulikuwa tukikishirikisha katika ibada ya Mwenyezi Mungu.» info
التفاسير:

external-link copy
85 : 40

فَلَمۡ يَكُ يَنفَعُهُمۡ إِيمَٰنُهُمۡ لَمَّا رَأَوۡاْ بَأۡسَنَاۖ سُنَّتَ ٱللَّهِ ٱلَّتِي قَدۡ خَلَتۡ فِي عِبَادِهِۦۖ وَخَسِرَ هُنَالِكَ ٱلۡكَٰفِرُونَ

Imani yao hiyo haikuwa ni yenye kuwanufaisha walipoiona adhabu yetu, kwa kuwa ni imani ambayo hawakuwa na budi nayo, na si Imani ya hiyari na kutaka. Huo ndio mpango na njia Aliyoiweka kwa ummah wote, kwamba Imani isiwanufaishe wanapoiona adhabu. Na itakapokuja adhabu ya Mwenyezi Mungu, wataangamia wenye kumkanusha Mola wao, wenye kukataa kumpwekesha na kumtii. info
التفاسير: