Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Əli Muhsin əl-Bərvani.

Al-Mursalat

external-link copy
1 : 77

وَٱلۡمُرۡسَلَٰتِ عُرۡفٗا

Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole! [1] info

[1] Naapa kwa Aya zilizo tumwa kwa ulimi wa Jibrili kumpelekea Muhammad kwa upole wa kawaida na kheri,

التفاسير:

external-link copy
2 : 77

فَٱلۡعَٰصِفَٰتِ عَصۡفٗا

Na zinazo vuma kwa kasi! [2] info

[2] Na kwa Aya zenye kuzitwaa kwa nguvu dini nyengine zote za uwongo zikizipeperushia mbali,

التفاسير:

external-link copy
3 : 77

وَٱلنَّٰشِرَٰتِ نَشۡرٗا

Na zikaeneza maeneo yote! [3] info

[3] Na kwa Aya zenye kueneza hikima na uwongofu katika nyoyo za walimwengu kwa uenezi mkubwa mno,

التفاسير:

external-link copy
4 : 77

فَٱلۡفَٰرِقَٰتِ فَرۡقٗا

Na zinazo farikisha zikatawanya! [4] info

[4] Na zenye kufarikisha baina ya kweli na uwongo kwa mfarakano ulio wazi kabisa,

التفاسير:

external-link copy
5 : 77

فَٱلۡمُلۡقِيَٰتِ ذِكۡرًا

Na zinazo peleka mawaidha! [5] info

[5] Na zenye kuwapa watu mawaidha ya kuwanufaisha,

التفاسير:

external-link copy
6 : 77

عُذۡرًا أَوۡ نُذۡرًا

Kwa kuudhuru au kuonya, [6] info

[6] Ili iwe ni udhuru kwao na onyo wasiwe na hoja,

التفاسير:

external-link copy
7 : 77

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَٰقِعٞ

Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa! [7] info

[7] Hakika haya mliyo ahidiwa ya kuja Kiyama kwa yakini yatatimia tu bila ya shaka yoyote.

التفاسير:

external-link copy
8 : 77

فَإِذَا ٱلنُّجُومُ طُمِسَتۡ

Wakati nyota zitakapo futwa, [8] info

[8] Basi nyota zitapo ondolewa kabisa,

التفاسير:

external-link copy
9 : 77

وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ فُرِجَتۡ

Na mbingu zitakapo pasuliwa, [9] info

[9] Na mbingu zitapo pasuka,

التفاسير:

external-link copy
10 : 77

وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ نُسِفَتۡ

Na milima itakapo peperushwa, [10] info

[10] Na milima ikavurugwa na ikapeperushiwa mbali na upepo,

التفاسير:

external-link copy
11 : 77

وَإِذَا ٱلرُّسُلُ أُقِّتَتۡ

Na Mitume watakapo wekewa wakati wao, [11] info

[11] Na Mitume wakawekewa wakati maalumu wahudhurie kwa ajili ya kuwatolea ushahidi kaumu zao.

التفاسير:

external-link copy
12 : 77

لِأَيِّ يَوۡمٍ أُجِّلَتۡ

Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo? [12] info

[12] Kwa ajili ya siku gani yametayarishwa mambo haya makubwa makubwa?

التفاسير:

external-link copy
13 : 77

لِيَوۡمِ ٱلۡفَصۡلِ

Kwa siku ya kupambanua! [13] info

[13] Kwa ajili ya siku watakapo pambanuliwa baina ya viumbe.

التفاسير:

external-link copy
14 : 77

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ

Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini? [14] info

[14] Na nini cha kukujuvya ina nini hiyo siku ya kupambanua?

التفاسير:

external-link copy
15 : 77

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha! [15] info

[15] Ni maangamio ya milele siku hiyo kwa hao wanao kadhibisha walio waahidi Mitume!

التفاسير:

external-link copy
16 : 77

أَلَمۡ نُهۡلِكِ ٱلۡأَوَّلِينَ

Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia? [16] info

[16] Kwani hatukuwaangamiza mataifa ya zamani yaliyo kadhibisha,

التفاسير:

external-link copy
17 : 77

ثُمَّ نُتۡبِعُهُمُ ٱلۡأٓخِرِينَ

Kisha tukawafuatilizia walio fuatia? [17] info

[17] Na kisha tukawafuatilizia hao wenginewe tukawateketeza hali kadhaalika,

التفاسير:

external-link copy
18 : 77

كَذَٰلِكَ نَفۡعَلُ بِٱلۡمُجۡرِمِينَ

Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu! [18] info

[18] Kwa madhambi waliyo yafanya na walivyo mkataa Mwenyezi Mungu?

التفاسير:

external-link copy
19 : 77

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! [19] info

[19] Siku hiyo ni siku ya kuteketezwa walio kadhibisha, kama tulivyo waahidi.

التفاسير: