Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Əli Muhsin əl-Bərvani.

Səhifənin rəqəmi:close

external-link copy
38 : 12

وَٱتَّبَعۡتُ مِلَّةَ ءَابَآءِيٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَۚ مَا كَانَ لَنَآ أَن نُّشۡرِكَ بِٱللَّهِ مِن شَيۡءٖۚ ذَٰلِكَ مِن فَضۡلِ ٱللَّهِ عَلَيۡنَا وَعَلَى ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَشۡكُرُونَ

Na nimefuata mila ya baba zangu, Ibrahim, na Is-haq, na Yaa'qub. Hatuna haki ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote. Hiyo ni katika fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yetu na juu ya watu; lakini watu wengi hawashukuru. info

Mimi nimeacha mila ya hawa makafiri, na nikafuata Dini ya baba zangu Ibrahim, na Is-haaq, na Yaa'qub. Nikamuabudu Mwenyezi Mungu pekee. Haitufalii sisi kumfanyia Mwenyezi Mungu mshirika yeyote yule, akiwa Malaika, au jini, au mwanaadamu, licha ya masanamu ambayo hayaleti manufaa wala madhara, wala hayasikii, wala hayaoni! Hiyo ndiyo Tawhidi aliyo tutunukia Mwenyezi Mungu sisi na watu wote, kwa vile alivyo tuamrisha tuwafikilishie ujumbe. Lakini wengi wa watu hawaipokei fadhila hii kwa shukrani, bali wanaikataa!

التفاسير:

external-link copy
39 : 12

يَٰصَٰحِبَيِ ٱلسِّجۡنِ ءَأَرۡبَابٞ مُّتَفَرِّقُونَ خَيۡرٌ أَمِ ٱللَّهُ ٱلۡوَٰحِدُ ٱلۡقَهَّارُ

Enyi wafungwa wenzangu wawili! Je, mabwana wengi wanao farikiana wao kwa wao ni bora au Mwenyezi Mungu Mmoja Mwenye nguvu? info

Enyi wenzangu wawili wa gerezani! Je mabwana wengi mbali mbali ni bora mtu kuwanyenyekea kuliko Mwenyezi Mungu Mmoja asiye shindika?

التفاسير:

external-link copy
40 : 12

مَا تَعۡبُدُونَ مِن دُونِهِۦٓ إِلَّآ أَسۡمَآءٗ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٍۚ إِنِ ٱلۡحُكۡمُ إِلَّا لِلَّهِ أَمَرَ أَلَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّآ إِيَّاهُۚ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلۡقَيِّمُ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ

Hamuabudu badala yake ila majina tu mliyo yapanga nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuyateremshia hayo uthibitisho wowote. Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini Iliyo Nyooka. Lakini watu wengi hawajui. info

Hamuabudu badala ya Mwenyezi Mungu ila majina tu mliyo yazua nyinyi na baba zenu kwa mawazo bila ya kuwepo kweli. Mwenyezi Mungu hakuwateremshia hao hoja wala ushahidi wowote! Hapana wa kuhukumu nini kinacho faa kuabudiwa na kipi hakifai ila Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimnyenyekee yeyote mwenginewe, na mumuabudu Yeye peke yake. Hiyo ndiyo Dini iliyo nzima iliyo nyooka, ambayo dalili zote na ushahidi unaelekea kwake. Lakini aghlabu ya watu hawataki uwongozi wa dalili hizi, wala hawajijui kuwa wamo katika ujinga na upotovu.

التفاسير:

external-link copy
41 : 12

يَٰصَٰحِبَيِ ٱلسِّجۡنِ أَمَّآ أَحَدُكُمَا فَيَسۡقِي رَبَّهُۥ خَمۡرٗاۖ وَأَمَّا ٱلۡأٓخَرُ فَيُصۡلَبُ فَتَأۡكُلُ ٱلطَّيۡرُ مِن رَّأۡسِهِۦۚ قُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ ٱلَّذِي فِيهِ تَسۡتَفۡتِيَانِ

Enyi wafungwa wenzangu wawili! Ama mmoja wenu atamnywesha bwana wake mvinyo. Na ama mwengine atasulubiwa, na ndege watamla kichwa chake. Imekwisha katwa hukumu ya hilo jambo mlilo kuwa mkiuliza. info

Enyi wenzangu wawili wa gerezani! Hii basi ndiyo tafsiri ya ndoto zenu: Ama mmoja wenu aliye kamua zabibu katika ndoto yake, atatoka jela, na atakuwa akimnywesha mvinyo Mfalme. Na ama huyu wa pili atatundikwa msalabani, na ataachwa msalabani ndege wakimla kichwa chake. Yamekwisha timia hayo mambo kama nilivyo eleza kwa mujibu mlivyo nitaka nieleze tafsiri ya hizo ndoto!

التفاسير:

external-link copy
42 : 12

وَقَالَ لِلَّذِي ظَنَّ أَنَّهُۥ نَاجٖ مِّنۡهُمَا ٱذۡكُرۡنِي عِندَ رَبِّكَ فَأَنسَىٰهُ ٱلشَّيۡطَٰنُ ذِكۡرَ رَبِّهِۦ فَلَبِثَ فِي ٱلسِّجۡنِ بِضۡعَ سِنِينَ

Na akamwambia yule aliye jua kuwa atavuka katika wale wawili: Nikumbuke kwa bwana wako. Lakini Shet'ani alimsahaulisha kumtaja kwa bwana wake. Basi Yusuf akakaa gerezani miaka kadhaa. info

Akamwambia yule aliye kuwa atavuka: Nitaje kwa Mfalme kwa sifa zangu, na kisa changu. Asaa huenda akanifanyia insafu akanivua na haya mateso! Shetani alimshughulisha akamsahaulisha kutaja kisa cha Yusuf kwa Mfalme. Basi Yusuf akabaki gerezani kwa miaka isiyo pungua mitatu.

التفاسير:

external-link copy
43 : 12

وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ إِنِّيٓ أَرَىٰ سَبۡعَ بَقَرَٰتٖ سِمَانٖ يَأۡكُلُهُنَّ سَبۡعٌ عِجَافٞ وَسَبۡعَ سُنۢبُلَٰتٍ خُضۡرٖ وَأُخَرَ يَابِسَٰتٖۖ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمَلَأُ أَفۡتُونِي فِي رُءۡيَٰيَ إِن كُنتُمۡ لِلرُّءۡيَا تَعۡبُرُونَ

Na siku moja mfalme alisema: Hakika mimi nimeota ng'ombe saba wanene wanaliwa na ng'ombe saba walio konda. Na mashuke saba mabichi na mengine makavu. Enyi waheshimiwa! Nambieni maana ya ndoto zangu, ikiwa nyinyi mnaweza kuagua ndoto. info

Mfalme akasema: Nimeota usingizini kuna ng'ombe saba wanene wanaliwa na wengine saba walio konda madhaifu. Na nimeota mashuke saba mabichi, na mengine saba makavu. Enyi wakuu wanazuoni na wenye maarifa! Nitoleeni fatwa ya hizi ndoto zangu, ikiwa ni kweli nyinyi mnajua tafsiri za ndoto na mnaweza kuzitolea fatwa.

التفاسير: