Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Abdullah Məhəmməd və Nasir Xamis.

Səhifənin rəqəmi:close

external-link copy
78 : 5

لُعِنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۢ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُۥدَ وَعِيسَى ٱبۡنِ مَرۡيَمَۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَواْ وَّكَانُواْ يَعۡتَدُونَ

Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anatoa habari kwamba Amewafukuza kutoka kwenye rehema Yake makafiri miongoni mwa Wana wa Isrāīl, kama ilivyoandikwa kwenye kitabu ambacho Mwenyezi Mungu Alikiteremsha kwa Dāwūd, amani imshukie, nacho ni Zaburi, na kwenye kitabu Alichokiteremsha kwa Īsā, amani imshukie, nacho ni Injili, kwa sababu ya kuasi kwao na kuyafanyia uadui kwao mambo Aliyoyatukuza Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. info
التفاسير:

external-link copy
79 : 5

كَانُواْ لَا يَتَنَاهَوۡنَ عَن مُّنكَرٖ فَعَلُوهُۚ لَبِئۡسَ مَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ

Walikuwa, Mayahudi hawa, wakiyafanya maasia waziwazi, wakiridhika nayo na hawakuwa wakikatazana wao kwa wao maovu yoyote waliyoyafanya. Na hili ni katika vitendo vyao viovu. Na kwa hilo walistahiki kufukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. info
التفاسير:

external-link copy
80 : 5

تَرَىٰ كَثِيرٗا مِّنۡهُمۡ يَتَوَلَّوۡنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۚ لَبِئۡسَ مَا قَدَّمَتۡ لَهُمۡ أَنفُسُهُمۡ أَن سَخِطَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡ وَفِي ٱلۡعَذَابِ هُمۡ خَٰلِدُونَ

Utawaona, ewe Mtume, wengi wa hawa Mayahudi wanawafanya washirikina kuwa ni wategemewa wao. Ni baya mno hilo walilolifanya la mshikamano huo uliokuwa ni sababu ya kukasirikiwa kwao na Mwenyezi Mungu na kukaa kwao milele kwenye adhabu ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
81 : 5

وَلَوۡ كَانُواْ يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلنَّبِيِّ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِ مَا ٱتَّخَذُوهُمۡ أَوۡلِيَآءَ وَلَٰكِنَّ كَثِيرٗا مِّنۡهُمۡ فَٰسِقُونَ

Na lau hawa Mayahudi ambao wanasaidiana na washirikina walikuwa wamemuamini Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na Mtume Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na wakayakubali yale yaliyoteremshwa kwake, nayo ni Qur’ani tukufu, hawangaliwafanya makafiri kuwa ni marafiki na waokozi. Lakini wengi katika wao wako nje ya twaa ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. info
التفاسير:

external-link copy
82 : 5

۞ لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ ٱلنَّاسِ عَدَٰوَةٗ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱلۡيَهُودَ وَٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْۖ وَلَتَجِدَنَّ أَقۡرَبَهُم مَّوَدَّةٗ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّا نَصَٰرَىٰۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنۡهُمۡ قِسِّيسِينَ وَرُهۡبَانٗا وَأَنَّهُمۡ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ

Utakuta tena utakuta, ewe Mtume, kwamba watu wenye uadui mno kwa wale waliokukubali wakakuamini na wakakufuata ni Mayahudi, kwa sababu ya ukaidi wao, ukanushaji wao na kuichukia kwao haki, na wale wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu kingine, kama wanaoabudu masanamu na wengineo. Na utakuta tena utakuta kwamba walio karibu mno kimapenzi na Waislamu ni wale waliosema, «Sisi ni Wanaswara.» Hilo ni kwamba miongoni mwao kuna wasomi wanaoijua dini yao, wacha-Mungu, wanaofanya jitihadi ya ibada kwenye mindule, na kwamba wao ni wanyenyekevu, hawafanyi kiburi cha kutiubali haki. Hao ndio wale walioukubali ujumbe wa Mtume Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na wakauamini. info
التفاسير:

external-link copy
83 : 5

وَإِذَا سَمِعُواْ مَآ أُنزِلَ إِلَى ٱلرَّسُولِ تَرَىٰٓ أَعۡيُنَهُمۡ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمۡعِ مِمَّا عَرَفُواْ مِنَ ٱلۡحَقِّۖ يَقُولُونَ رَبَّنَآ ءَامَنَّا فَٱكۡتُبۡنَا مَعَ ٱلشَّٰهِدِينَ

Na miongoni mwa yale yanayoonyesha mapenzi yao kwa Waislamu ni kuwa kundi katika wao (nao ni tume ya watu wa Habashah walipoisikia Qur’ani) yalibubujika machozi macho yao wakawa na yakini kuwa hiyo ni haki iliyoteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, wakamuamini Mwenyezi Mungu, wakamfuata Mtume Wake na wakanyenyekea kwa Mwenyezi Mungu wakimuomba awatukuze kwa heshima ya kushirikiana na umati wa Muhammad, amani imshukie, katika kuwatolea ushahidi umma wengine Siku ya Kiyama. info
التفاسير: