Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Abdullah Məhəmməd və Nasir Xamis.

Səhifənin rəqəmi:close

external-link copy
128 : 4

وَإِنِ ٱمۡرَأَةٌ خَافَتۡ مِنۢ بَعۡلِهَا نُشُوزًا أَوۡ إِعۡرَاضٗا فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡهِمَآ أَن يُصۡلِحَا بَيۡنَهُمَا صُلۡحٗاۚ وَٱلصُّلۡحُ خَيۡرٞۗ وَأُحۡضِرَتِ ٱلۡأَنفُسُ ٱلشُّحَّۚ وَإِن تُحۡسِنُواْ وَتَتَّقُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٗا

Na mwanamke akijua kuwa mumewe ana majivuno na madharau na hashughuliki naye, si makosa kwa wao wawili kusikilizana kwa namana ya kuwaridhisha wao wawili kuhusu kugawa siku na matumizi. Kwani masikilizano ni bora zaidi na ni afadhali zaidi. Na nafsi zimeumbwa zikiwa na tabia ya pupa na ubahili, kama kwamba ubahili upo mbele ya hizo nafsi, hauepukani nazo. Na mkiamiliana na wake wenu vizuri na mkamcha Mwenyezi Mungu juu yao, basi Mwenyezi Mungu ni Mjuzi sana wa mnayoyafanya, katika hayo na mengineyo, hakuna kinachofichika Kwake, na Atawalipa kwa hayo. info
التفاسير:

external-link copy
129 : 4

وَلَن تَسۡتَطِيعُوٓاْ أَن تَعۡدِلُواْ بَيۡنَ ٱلنِّسَآءِ وَلَوۡ حَرَصۡتُمۡۖ فَلَا تَمِيلُواْ كُلَّ ٱلۡمَيۡلِ فَتَذَرُوهَا كَٱلۡمُعَلَّقَةِۚ وَإِن تُصۡلِحُواْ وَتَتَّقُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا

Na hamtaweza, enyi wanaume, kuhakikisha uadilifu kamili wa mapenzi na muelekeo wa moyo kati ya wanawake, namna mtakavyofanya bidii juu ya hilo. Basi msimpe mgongo, yule msiokuwa na haja naye, kabisa-kabisa mkamuacha akawa ni kama mwanamke ambaye hana mume wala hakutalikiwa, mkaja mkapata madhambi. Na mkizitengeneza amali zenu mkafanya uadilifu katika ugawaji wenu baina ya wake zenu na mkamchunga Mwenyezi Mungu mkamuogopa juu yao, basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake, ni Mwingi wa huruma kwao. info
التفاسير:

external-link copy
130 : 4

وَإِن يَتَفَرَّقَا يُغۡنِ ٱللَّهُ كُلّٗا مِّن سَعَتِهِۦۚ وَكَانَ ٱللَّهُ وَٰسِعًا حَكِيمٗا

Na ukitokea utengano baina ya mwanamume na mkewe, Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, atamtosheleza kila mmoja kati yao kwa fadhila Zake na ukunjufu wa neema Zake. Kwani Yeye, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu na Aliyetukuka, ni Mkunjufu wa fadhila na neema, ni Mwingi wa hekima katika hukumu Zake Anazozipitisha kwa waja Wake. info
التفاسير:

external-link copy
131 : 4

وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَلَقَدۡ وَصَّيۡنَا ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكُمۡ وَإِيَّاكُمۡ أَنِ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ وَإِن تَكۡفُرُواْ فَإِنَّ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَنِيًّا حَمِيدٗا

Ni milki ya Mwenyezi Mungu vilivyoko kwenye mbingu na vilivyoko kwenye ardhi na vilivyoko baina ya hivyo viwili. Na tuliwausia wale waliopewa Vitabu kabla yenu, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, na tukawausia nyinyi pia, enyi ummah wa Muhammad, mumche Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na msimame kutekeleza amri Zake na kuepuka makatazo Yake, na tukawaelezea kwamba nyinyi mkiukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na sheria Zake, basi Mwenyezi Mungu Hawahitajii nyinyi, kwa kuwa vyote vilivyoko kwenye mbingu na vilivyoko kwenye ardhi ni Vyake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha kutowahitjia viumbe Wake, ni Mwingi wa kuhimidiwa katika sifa Zake na vitendo Vyake. info
التفاسير:

external-link copy
132 : 4

وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلًا

Ni milki ya Mwenyezi Mungu viumbe vilivyoko katika ulimwengu huu. Na inatosha kuwa Yeye, Aliyetakasika na kila sifa pungufu, ni Msimamizi na Mtunzi wa mambo ya viumbe Vyake. info
التفاسير:

external-link copy
133 : 4

إِن يَشَأۡ يُذۡهِبۡكُمۡ أَيُّهَا ٱلنَّاسُ وَيَأۡتِ بِـَٔاخَرِينَۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ قَدِيرٗا

Akitaka Mwenyezi Mungu Atawaangamiza, enyi watu, na awalete watu wengine wasiokuwa nyinyi. Na Mwenyezi Mungu kwa hili ni Muweza. info
التفاسير:

external-link copy
134 : 4

مَّن كَانَ يُرِيدُ ثَوَابَ ٱلدُّنۡيَا فَعِندَ ٱللَّهِ ثَوَابُ ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ سَمِيعَۢا بَصِيرٗا

Mwenye kuwa na hamu miongoni mwenu, enyi watu, ya kupata malipo ya duniani na akaipa mgongo Akhera, basi mbele ya Mwenyezi Mungu kuna malipo ya dunia na Akhera. Basi na atake kutoka kwa Mwenyezi Mungu , Peke Yake, wema wa dunia na Akhera, kwani Yeye Ndiye Anayevimiliki hivyo viwili. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyasikia maneno ya waja Wake, ni Mwenye kuziona nia zao na vitendo vyao, na Atawalipa kwa hayo. info
التفاسير: