Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Abdullah Məhəmməd və Nasir Xamis.

Səhifənin rəqəmi:close

external-link copy
122 : 4

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ سَنُدۡخِلُهُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۖ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٗاۚ وَمَنۡ أَصۡدَقُ مِنَ ٱللَّهِ قِيلٗا

Na wale waliokuwa wakweli katika kumuamini kwao Mwenyezi Mungu, Aliyetukua, na wakafuatanisha Imani yao na matendo mema, basi Mwenyezi Mungu Atawaingiza, kwa ukarimu Wake, ndani ya mabustani ya Pepo ambayo chini ya majumba yake ya fahari na miti yake inapita mito, hali ya kukaa milele humo. Hiyo ni ahadi inayotoka kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ambaye Haendi kinyume na ahadi Yake. Na hapana yoyote aliye mkweli zaidi, katika neno lake na ahadi yake, kuliko Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. info
التفاسير:

external-link copy
123 : 4

لَّيۡسَ بِأَمَانِيِّكُمۡ وَلَآ أَمَانِيِّ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِۗ مَن يَعۡمَلۡ سُوٓءٗا يُجۡزَ بِهِۦ وَلَا يَجِدۡ لَهُۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرٗا

Fadhila hizi kubwa hazipatikani kwa matamanio mnayoyatamani, enyi Waislamu, wala kwa matamanio ya Mayahudi na Wanaswara waliopewa Kitabu. Hakika zinapatikana kwa kumuamini Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kikweli na kuyafanya vizuri matendo ya kumridhisha. Na yoyote mwenye kufanya tendo baya, atalipwa kwalo, na hatompata, asiyekuwa Mwenyezi Mungu, mtegemewa mwenye kusimamia mambo yake wala msaidizi mwenye kumnusuru na kumuepushia adhabu mbaya. info
التفاسير:

external-link copy
124 : 4

وَمَن يَعۡمَلۡ مِنَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ مِن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَأُوْلَٰٓئِكَ يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ وَلَا يُظۡلَمُونَ نَقِيرٗا

Na mwenye kufanya matendo mema, awe ni mwanamume au mwanamke, hali ya kuwa anamuamini Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na haki Aliyoiteremsha, basi hao Mwenyezi Mungu Atawaingiza Peponi, nyumba ya starahe ya daima, na hawatopunguziwa chochote katika thawabu za matendo yao, hata kama ni kadiri ya kitone kilichoko kwenye koko ya tende. info
التفاسير:

external-link copy
125 : 4

وَمَنۡ أَحۡسَنُ دِينٗا مِّمَّنۡ أَسۡلَمَ وَجۡهَهُۥ لِلَّهِ وَهُوَ مُحۡسِنٞ وَٱتَّبَعَ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۗ وَٱتَّخَذَ ٱللَّهُ إِبۡرَٰهِيمَ خَلِيلٗا

Hakuna yoyote aliye mwema wa dini kuliko yule aliyejisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Peke Yake, kwa moyo wake na viungo vyake vyote, hali ya kuwa ni mwema wa maneno na vitendo, mwenye kufuata amri ya Mola wake, akawa amefuata mila ya Ibrāhīm na Sheria aliyoileta na amejiepusha na itikadi mbaya na sheria zilizo batili. Na Mwenyezi Mungu Alimteua Ibrāhīm, rehema na amani zimshukiye, na Akamfanya ni msafiwa Wake miongoni mwa viumbe Wake. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya al-khullah (ubui) kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, nao ni daraja ya juu kabisa ya mapenzi na uteuzi. info
التفاسير:

external-link copy
126 : 4

وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٖ مُّحِيطٗا

Ni vya Mwenyezi Mungu viumbe vyote vilivyoko ulimwenguni. Hivyo ni milki Yake, Aliyetukuka, Peke Yake. Na Mwenyezi Mungu Amekizunguka kila kitu, hakuna kitu chochote, katika mambo ya waja Wake, chenye kufichika Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
127 : 4

وَيَسۡتَفۡتُونَكَ فِي ٱلنِّسَآءِۖ قُلِ ٱللَّهُ يُفۡتِيكُمۡ فِيهِنَّ وَمَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡكُمۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ فِي يَتَٰمَى ٱلنِّسَآءِ ٱلَّٰتِي لَا تُؤۡتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرۡغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ وَٱلۡمُسۡتَضۡعَفِينَ مِنَ ٱلۡوِلۡدَٰنِ وَأَن تَقُومُواْ لِلۡيَتَٰمَىٰ بِٱلۡقِسۡطِۚ وَمَا تَفۡعَلُواْ مِنۡ خَيۡرٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِهِۦ عَلِيمٗا

Watu wanakutaka, ewe Nabii, uwaelezee mambo yaliyowatatiza kuyafahamu yanayowahusu wanawake na hukumu zao. Sema, «Mwenyezi Mungu Anawafafanulia kuhusu mambo yao na yale mnayosomewa ndani ya Qur’ani kuhusu mayatima wa kike ambao hamuwapi mafungu yao waliyoandikiwa na Mwenyezi Mungu ya mahari, mirathi na haki nyiginezo, na mkawa mnapenda kuwaoa au hamuna hamu ya kuwaoa. Na pia Mwenyezi Mungu Anawafafanulia kuhusu mambo ya madhaifu miongoni mwa watoto na ulazima wa kuwasimamia mayatima kwa uadilifu na kuacha kuwafanyia maonevu kwa kuwanyima haki zao. Na wema wowote mnaoufanya, Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anaujua, hakuna kinachofichika Kwake kuhuso huo na mwengineo. info
التفاسير: