আল-কোৰআনুল কাৰীমৰ অৰ্থানুবাদ - শ্বাহিলি অনুবাদ- আলী মুহছিন আল-বাৰওৱানী

পৃষ্ঠা নং:close

external-link copy
84 : 5

وَمَا لَنَا لَا نُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَمَا جَآءَنَا مِنَ ٱلۡحَقِّ وَنَطۡمَعُ أَن يُدۡخِلَنَا رَبُّنَا مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلصَّٰلِحِينَ

Na kwa nini tusimuamini Mwenyezi Mungu na Haki iliyo tujia, na hali tunatumai Mola wetu Mlezi atuingize pamoja na watu wema? info

Na nini cha kutuzuia tusimsadiki Mwenyezi Mungu peke yake, na Haki iliyo teremka kwa Muhammad? Na hali sisi tunamtaraji Mwenyezi Mungu atuingize Peponi pamoja na watu wenye Imani njema na vitendo vyema.

التفاسير:

external-link copy
85 : 5

فَأَثَٰبَهُمُ ٱللَّهُ بِمَا قَالُواْ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ وَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Basi Mwenyezi Mungu atawalipa, kwa yale waliyo yasema, Bustani zipitazo mito katika yake; humo watadumu. Na haya ndiyo malipo ya wafanyao wema. info

Kwa hivyo Mwenyezi Mungu amewaandikia malipo kwa vile kuungama kwao, nayo ni Bustani yenye kupita mito chini ya miti yake, na majumba ya fakhari ya kukaa humo daima, pamoja na watu ambao ni njema itikadi zao na vitendo vyao.

التفاسير:

external-link copy
86 : 5

وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَحِيمِ

Na wale walio kufuru na wakazikanusha Ishara zetu, hao ndio watu wa Motoni. info

Na walio mpinga Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wakazikanya dalili alizo wateremshia kuwa ni uwongofu wa kufikia Haki, ni wao peke yao wanao stahiki adhabu kali katika Jahannamu.

التفاسير:

external-link copy
87 : 5

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُحَرِّمُواْ طَيِّبَٰتِ مَآ أَحَلَّ ٱللَّهُ لَكُمۡ وَلَا تَعۡتَدُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُعۡتَدِينَ

Enyi mlio amini! Msiharimishe vizuri alivyo kuhalalishieni Mwenyezi Mungu, wala msikiuke mipaka. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wakiukao mipaka. info

Enyi mlio amini! Msijiharimishie nafsi zenu vitu vizuri alivyo kuhalalishieni Mwenyezi Mungu, wala msipite mipaka aliyo kuwekeeni Mwenyezi Mungu ya kufuata mambo ya wastani. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi watu wanao pindukia mipaka.

التفاسير:

external-link copy
88 : 5

وَكُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ حَلَٰلٗا طَيِّبٗاۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ ٱلَّذِيٓ أَنتُم بِهِۦ مُؤۡمِنُونَ

Na kuleni katika alivyo kuruzukuni Mwenyezi Mungu, halali na vizuri. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mnamuamini. info

Na kuleni vitu alivyo kupeni Mwenyezi Mungu na akavifanya vyepesi kwenu, na akavifanya ni halali na ni vizuri kwa nafsi zenu. Na daima mwogopeni Mwenyezi Mungu, na mt'iini Yeye maadamu nyinyi mnamuamini Yeye.

التفاسير:

external-link copy
89 : 5

لَا يُؤَاخِذُكُمُ ٱللَّهُ بِٱللَّغۡوِ فِيٓ أَيۡمَٰنِكُمۡ وَلَٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ ٱلۡأَيۡمَٰنَۖ فَكَفَّٰرَتُهُۥٓ إِطۡعَامُ عَشَرَةِ مَسَٰكِينَ مِنۡ أَوۡسَطِ مَا تُطۡعِمُونَ أَهۡلِيكُمۡ أَوۡ كِسۡوَتُهُمۡ أَوۡ تَحۡرِيرُ رَقَبَةٖۖ فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ ثَلَٰثَةِ أَيَّامٖۚ ذَٰلِكَ كَفَّٰرَةُ أَيۡمَٰنِكُمۡ إِذَا حَلَفۡتُمۡۚ وَٱحۡفَظُوٓاْ أَيۡمَٰنَكُمۡۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمۡ ءَايَٰتِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Mwenyezi Mungu hatakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakushikeni kwa mnavyo apa kweli kweli kwa makusudio. Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa chakula cha wastani mnacho walisha ahali zenu, au kuwavisha, au kumkomboa mtumwa. Asiye pata hayo, basi afunge siku tatu. Hii ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapo apa. Na hifadhini yamini zenu. Namna hivyo Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake ili mpate kushukuru. info

Mwenyezi Mungu hakutiini adabu kwa sababu ya kuapa kiapo msicho kusudia. Bali hakika Yeye hukutieni adabu kwa sababu ya kuvunja viapo mlivyo vikusudia na yamini mliyo jifunga nayo. Basi ikiwa mmevunja kiapo itakupaseni mfanye jambo la kukughufirieni dhambi zake. Na mambo yenyewe ni: kuwalisha mafakiri kumi kwa siku moja, kwa chakula cha kawaida mnacho kila nyinyi na jamaa zenu mnao waangalia, yaani watu wenu wa nyumbani bila ya israfu wala ubakhili. Au kuwavika mafakiri kumi kwa kivazi kilicho zowewa. Au kumkomboa mtu kutoka utumwani. (Na mfano wa mtumwa ni mtu alioko kifungoni kwa dhulma, au chini ya utawala wa dhulma.) Ikiwa mwenye kuapa hawezi kutenda lolote katika hayo, basi itampasa afunge siku tatu. Na kila moja katika mambo haya hufuta dhambi za mwenye kuapa kiapo cha kutilia niya na akakivunja. Nanyi zilindeni yamini zenu, msiape katika mambo yasiyo kuwa laiki yake, na wala msiache kutenda kitendo cha kughufiria dhambi pindi mkivunja kiapo. Kwa mpango huu Mwenyezi Mungu anakufafanulieni hukumu zake ili mpate kushukuru neema zake kwa kuzijua na kuzifuata vilivyo. Katika hukumu ya yamini pana mawili yafaa tuyazingatie. Kwanza: Uislamu umeraghibisha sana kukomboa watumwa. Sababu nyingi zinazo wajibisha hayo. Kafara nyingi za dhambi zinahitaji kukomboa. Kafara ya kula mchana Ramadhani yahitaji ukombozi, n.k. Na katika hayo yanaonyesha Uislamu unachukia utumwa. Uislamu uliukiri utumwa kwa kuwa maadui wao walikuwa wakiwatia utumwani Waislamu, basi na Uislamu ukaruhusu kuwatendea wao vivyo hivyo. Pili: Uislamu unakazania kulisha masikini kila ikipatikana fursa.

التفاسير:

external-link copy
90 : 5

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّمَا ٱلۡخَمۡرُ وَٱلۡمَيۡسِرُ وَٱلۡأَنصَابُ وَٱلۡأَزۡلَٰمُ رِجۡسٞ مِّنۡ عَمَلِ ٱلشَّيۡطَٰنِ فَٱجۡتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ

Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa. info

Enyi wenye kumsadiki Mwenyezi Mungu na Vitabu vyake na Mitume wake, wenye kuifuata Haki! Kunywa au kuvuta chochote kinacho lewesha, kucheza kamari, na kusimamisha mawe ya kutolea mihanga kwa ajili ya masanamu mnayo yaabudu, na kuagua kwa mishale, na mawe, na karatasi za kuagulia kudra iliyo ghaibu...yote hayo si chochote ila ni uchafu wa kiroho, na upotovu. Na hayo ni kupambiwa na Shetani tu. Basi yaachilieni mbali ili mpate kufuzu duniani kwa maisha bora, na Akhera mpate Janna yenye neema. Kuagua kwa mishale: ilikuwa ikiandikwa juu ya vijiti, kimoja kiliandikwa: "Mola wangu Mlezi kaniamuru", na kingine:"Mola wangu Mlezi kanikataza", na kingine hakikuandikwa kitu. Hutiwa vijiti hivyo katika mfuko kisha huchanganywa, na kohani hutia mkono wake akachomoa kimojapo, na akamjuvya mwenye kuuliza lilio aguliwa

التفاسير: