የቅዱስ ቁርዓን ይዘት ትርጉም - የስዋሒሊኛ ትርጉም - በዐሊይ ሙሕሲን አል-በርዋኒይ

At-Takathur

external-link copy
1 : 102

أَلۡهَىٰكُمُ ٱلتَّكَاثُرُ

Kumekushughulisheni kutafuta wingi, info

Yamekushughulisheni mkaacha kutimiza yaliyo waajibu na ya ut'iifu kule kujitapa kwenu kwa wana na wafwasi, na kujifakhiri kwa mali, na hisabu, na nasaba, mpaka yakusibuni mauti!

التفاسير:

external-link copy
2 : 102

حَتَّىٰ زُرۡتُمُ ٱلۡمَقَابِرَ

Mpaka mje makaburini! info

Mpaka yakusibuni mauti!

التفاسير:

external-link copy
3 : 102

كَلَّا سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ

Sivyo hivyo! Mtakuja jua! info

Hakika mtakuja jua matokeo ya upumbavu wenu na mapuuza yenu.

التفاسير:

external-link copy
4 : 102

ثُمَّ كَلَّا سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ

Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua! info

Na hakika bila ya shaka mtakuja jua natija ya hayo!

التفاسير:

external-link copy
5 : 102

كَلَّا لَوۡ تَعۡلَمُونَ عِلۡمَ ٱلۡيَقِينِ

Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini, info

Ama kwa hakika lau mngeli jua kwa yakini uovu wa mwisho wenu bila ya shaka mngeli ogopa huko kushindania kurindika mali, na mngeli jitengenezea Akhera yenu.

التفاسير:

external-link copy
6 : 102

لَتَرَوُنَّ ٱلۡجَحِيمَ

Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu! info

Nakuapieni na nakutilieni mkazo, enyi watu, kwamba hakika nyinyi mtakuja ushuhudia Moto unao waka.

التفاسير:

external-link copy
7 : 102

ثُمَّ لَتَرَوُنَّهَا عَيۡنَ ٱلۡيَقِينِ

Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini. info

Kisha ninaapa na natilia mkazo kwamba mtauona wazi na kwa yakini.

التفاسير:

external-link copy
8 : 102

ثُمَّ لَتُسۡـَٔلُنَّ يَوۡمَئِذٍ عَنِ ٱلنَّعِيمِ

Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema. info

Tena naapa na natilia mkazo kwamba hakika nyinyi mtahisabiwa kwa neema mlizo deka nazo na mkazistarehea.

التفاسير: