ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني
سورة التكاثر - At-Takathur
1:102
أَلۡهَىٰكُمُ ٱلتَّكَاثُرُ
Kumekushughulisheni kutafuta wingi,
Yamekushughulisheni mkaacha kutimiza yaliyo waajibu na ya ut'iifu kule kujitapa kwenu kwa wana na wafwasi, na kujifakhiri kwa mali, na hisabu, na nasaba, mpaka yakusibuni mauti!
التفاسير:
2:102
حَتَّىٰ زُرۡتُمُ ٱلۡمَقَابِرَ
Mpaka mje makaburini!
Mpaka yakusibuni mauti!
التفاسير:
3:102
كَلَّا سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ
Sivyo hivyo! Mtakuja jua!
Hakika mtakuja jua matokeo ya upumbavu wenu na mapuuza yenu.
التفاسير:
4:102
ثُمَّ كَلَّا سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ
Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua!
Na hakika bila ya shaka mtakuja jua natija ya hayo!
التفاسير:
5:102
كَلَّا لَوۡ تَعۡلَمُونَ عِلۡمَ ٱلۡيَقِينِ
Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini,
Ama kwa hakika lau mngeli jua kwa yakini uovu wa mwisho wenu bila ya shaka mngeli ogopa huko kushindania kurindika mali, na mngeli jitengenezea Akhera yenu.
التفاسير:
6:102
لَتَرَوُنَّ ٱلۡجَحِيمَ
Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu!
Nakuapieni na nakutilieni mkazo, enyi watu, kwamba hakika nyinyi mtakuja ushuhudia Moto unao waka.
التفاسير:
7:102
ثُمَّ لَتَرَوُنَّهَا عَيۡنَ ٱلۡيَقِينِ
Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini.
Kisha ninaapa na natilia mkazo kwamba mtauona wazi na kwa yakini.
التفاسير:
8:102
ثُمَّ لَتُسۡـَٔلُنَّ يَوۡمَئِذٍ عَنِ ٱلنَّعِيمِ
Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema.
Tena naapa na natilia mkazo kwamba hakika nyinyi mtahisabiwa kwa neema mlizo deka nazo na mkazistarehea.