《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼

页码:close

external-link copy
20 : 4

وَإِنۡ أَرَدتُّمُ ٱسۡتِبۡدَالَ زَوۡجٖ مَّكَانَ زَوۡجٖ وَءَاتَيۡتُمۡ إِحۡدَىٰهُنَّ قِنطَارٗا فَلَا تَأۡخُذُواْ مِنۡهُ شَيۡـًٔاۚ أَتَأۡخُذُونَهُۥ بُهۡتَٰنٗا وَإِثۡمٗا مُّبِينٗا

Na mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na hali mmoja wao mmempa chungu ya mali, basi msichukue katika hayo kitu chochote. Je, mtachukua kwa dhulma na kosa lilio wazi? info

Na pindi ikiwa mnataka kubadili mke pahala pa mke mwengine, na ikawa mmempa mmoja wao mali mengi basi si halali kwenu kuchukua chochote katika hayo. Jee mtachukua hayo kwa njia ya upotovu na kwa dhambi iliyo wazi?

التفاسير:

external-link copy
21 : 4

وَكَيۡفَ تَأۡخُذُونَهُۥ وَقَدۡ أَفۡضَىٰ بَعۡضُكُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٖ وَأَخَذۡنَ مِنكُم مِّيثَٰقًا غَلِيظٗا

Na mtachukuaje na ilhali mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti? info

Na vipi ikufalieni nyinyi kutaka kurudishiwa mahari mliyo kwisha yatoa, na hali mlikwisha changanyika nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wakafungamana nanyi kwa agano lenye nguvu ambalo kwalo Mwenyezi Mungu amewajibisha muingiane nao kwa ndoa.

التفاسير:

external-link copy
22 : 4

وَلَا تَنكِحُواْ مَا نَكَحَ ءَابَآؤُكُم مِّنَ ٱلنِّسَآءِ إِلَّا مَا قَدۡ سَلَفَۚ إِنَّهُۥ كَانَ فَٰحِشَةٗ وَمَقۡتٗا وَسَآءَ سَبِيلًا

Wala msiwaoe wake walio waoa baba zenu, ila yaliyo kwisha pita. Hakika huo ni uchafu na uchukizo na ni njia mbaya. info

Wala nyinyi, watoto, msiwaoe wanawake walio wahi kuolewa na baba zenu. Jambo hilo ni uchafu na linachusha, na linakirihiwa na Mwenyezi Mungu na watu. Na hiyo ni njia ovu kabisa. Lakini Mwenyezi Mungu anasamehe yaliyo kwisha tendeka katika zama za ujahili. Waarabu katika zama za ujahili walikuwa na ada zisio mpa heshima mwanamke, bali zikimdhulumu sana, na zikikata makhusiano mema katika ukoo. Ilikuwa mtu akifa baba yake na akawa na wake wasio kuwa mama yake mzazi, akilazimishwa kuwaoa, au akiwarithi wake za baba yake bila ya ndoa mpya. Na ilikuwa mtu akimwacha mke basi humpokonya kwa dhulma na uadui mahari yote aliyo mpa. Na walikuwapo walio kuwa wakimzuia huyo mt'laka asiolewe na mtu mwengine, kwa jeuri na inda. Ukaja Uislamu, ukamlinda mwanamke na dhulma hii iliyo wazi, ukakataza kurithiwa mke, na kumpokonya mahari yake hata chembe, ijapo kuwa ni mali mengi, na ukakataza kumzuia mt'alaka asiolewe, au kumkera ili apate kutaka yeye mke t'alaka kwa kutoa mali. Na katika mtindo wao Waarabu wa jahiliya ilikuwa yafaa mtu kumwoa aliye kuwa mke wa baba yake na akafarikiana naye kwa t'alaka au mfano wake. Uislamu ukakataza hayo, na ukauwita mtindo huo ni uchafu, kwa sababu ni jambo baya analo lichukia Mwenyezi Mungu na kila mwenye akili sawa. Huo ndio uadilifu wa Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
23 : 4

حُرِّمَتۡ عَلَيۡكُمۡ أُمَّهَٰتُكُمۡ وَبَنَاتُكُمۡ وَأَخَوَٰتُكُمۡ وَعَمَّٰتُكُمۡ وَخَٰلَٰتُكُمۡ وَبَنَاتُ ٱلۡأَخِ وَبَنَاتُ ٱلۡأُخۡتِ وَأُمَّهَٰتُكُمُ ٱلَّٰتِيٓ أَرۡضَعۡنَكُمۡ وَأَخَوَٰتُكُم مِّنَ ٱلرَّضَٰعَةِ وَأُمَّهَٰتُ نِسَآئِكُمۡ وَرَبَٰٓئِبُكُمُ ٱلَّٰتِي فِي حُجُورِكُم مِّن نِّسَآئِكُمُ ٱلَّٰتِي دَخَلۡتُم بِهِنَّ فَإِن لَّمۡ تَكُونُواْ دَخَلۡتُم بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ وَحَلَٰٓئِلُ أَبۡنَآئِكُمُ ٱلَّذِينَ مِنۡ أَصۡلَٰبِكُمۡ وَأَن تَجۡمَعُواْ بَيۡنَ ٱلۡأُخۡتَيۡنِ إِلَّا مَا قَدۡ سَلَفَۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا

Mmeharimishiwa mama zenu, na binti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na khaalati zenu, na binti wa ndugu mume, na binti wa dada, na mama zenu walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu walio zaliwa na wake zenu mlio waingilia. Ikiwa hamkuwaingilia basi hapana lawama juu yenu. (Pia mmeharimishwa) wake wa watoto wenu walio toka katika migongo yenu. Na kuwaoa pamoja dada wawili isipo kuwa yale yaliyo kwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. info

Mwenyezi Mungu amekuharimishieni kuwaoa mama zenu, na binti zenu, na dada zenu (ndugu wanawake) na shangazi zenu, na khaalati zenu (mama wadogo) na binti wa ndugu, na binti wa dada, na mama walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wakwe. Na walio harimishwa bila ya kunasibiana kwa damu ni: mama wa kunyonyesha, dada wa kunyonya, mama mkwe, binti za wake kwa waume wengine ikiwa hao wake wameingiliwa, na wake wa watoto mlio wazaa, na kuwaoa pamoja ndugu wawili. Yaliyo pita katika siku za ujahili yamesamehewa. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe kwa yaliyo pita kabla ya mpango huu, na Mwenye kuwarehemu katika aliyo kuwekeeni sharia. Ni Sharia ya Kiislamu pekee iliyo harimisha kwa sababu ya kunyonyesha. Anaye nyonya anakula kutokana na mwili wa mnyonyeshaji kama anavyo kula kutokana na mama yake ndani ya tumbo lake. Wote hao wawili wanakuwa ni sehemu yake huyo mtoto. Hapana khitilafu baina ya kukua ndani ya chumba na ndani ya tumbo. Na katika kuharimisha kwa kunyonyesha ni kumtukuza mnyonyeshaji, kwani anakuwa kama mama. Na haya ni kuzidi kushajiisha kunyonyesha kimaumbile, sio kwa chupa, kwa watoto wachanga.

التفاسير: