Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿里·穆哈辛·拜拉瓦尼

At-Tin

external-link copy
1 : 95

وَٱلتِّينِ وَٱلزَّيۡتُونِ

Naapa kwa tini na zaituni! info

Naapa kwa tini na zaituni, kwa baraka zao na ubora wa manufaa yao.

التفاسير:

external-link copy
2 : 95

وَطُورِ سِينِينَ

Na kwa Mlima wa Sinai! info

Na kwa mlima ambao juu yake ndio Mwenyezi Mungu alimsemeza Musa.

التفاسير:

external-link copy
3 : 95

وَهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ ٱلۡأَمِينِ

Na kwa mji huu wenye amani! info

Na kwa huu mji mtukufu wa Makka, ambao anaushuhudia utukufu wake mwenye kwenda uzuru, na anapata amani mwenye kuuingia.

التفاسير:

external-link copy
4 : 95

لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ فِيٓ أَحۡسَنِ تَقۡوِيمٖ

Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa. info

Kwa hakika bila ya shaka yoyote Sisi tumemuumba mtu amesimama sawa kwa umbo bora kabisa lilio nyooka, na akasifika kwa sifa nzuri kabisa.

التفاسير:

external-link copy
5 : 95

ثُمَّ رَدَدۡنَٰهُ أَسۡفَلَ سَٰفِلِينَ

Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini! info

Kisha tukamteremsha cheo mpaka akawa ni wa chini kabisa katika hao walioko chini, kwa kuacha kufanya waajibu wa hayo tuliyo muumbia.

التفاسير:

external-link copy
6 : 95

إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ فَلَهُمۡ أَجۡرٌ غَيۡرُ مَمۡنُونٖ

Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha. info

Lakini walio amini na wakatenda vitendo vyema, hao basi watapata ujira usio wakatikia wala kuwapungukia.

التفاسير:

external-link copy
7 : 95

فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعۡدُ بِٱلدِّينِ

Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo? info

Basi kitu gani kinacho kupelekea kukadhibisha kufufuliwa na kulipwa baada ya kuwekwa wazi uweza wetu wa hayo?

التفاسير:

external-link copy
8 : 95

أَلَيۡسَ ٱللَّهُ بِأَحۡكَمِ ٱلۡحَٰكِمِينَ

Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote? info

Kwani Mwenyezi Mungu aliye yatenda hayo tuliyo kueleza si muadilifu kuliko mahakimu wote kwa kufanya na kupanga?

التفاسير: