Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿里·穆哈辛·拜拉瓦尼

Al-Haqqah

external-link copy
1 : 69

ٱلۡحَآقَّةُ

Tukio la haki. info

Kiyama ni Tukio litakalo tukia kwa haki, yaani kwa kweli.

التفاسير:

external-link copy
2 : 69

مَا ٱلۡحَآقَّةُ

Nini hilo Tukio la haki? info

Nini hicho Kiyama kitacho tokea kweli?

التفاسير:

external-link copy
3 : 69

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحَآقَّةُ

Na nini kitakujuulisha nini hilo Tukio la haki? info

Na kitu gani kitacho kujuvya ukweli wake, na kitacho kupa sura ya kitisho chake na shida zake?

التفاسير:

external-link copy
4 : 69

كَذَّبَتۡ ثَمُودُ وَعَادُۢ بِٱلۡقَارِعَةِ

Thamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unao situsha. info

Kina Thamudi na kina A'di walikanusha Kiyama kinacho wagutua walimwengu wote kwa kitisho chake na shida zake.

التفاسير:

external-link copy
5 : 69

فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهۡلِكُواْ بِٱلطَّاغِيَةِ

Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno. info

Ama Thamudi basi walihilikiwa kwa tukio lilio pindukia mipaka yote kwa ukali wake.

التفاسير:

external-link copy
6 : 69

وَأَمَّا عَادٞ فَأُهۡلِكُواْ بِرِيحٖ صَرۡصَرٍ عَاتِيَةٖ

Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usio zuilika. info

Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo ubaridi na mkali,

التفاسير:

external-link copy
7 : 69

سَخَّرَهَا عَلَيۡهِمۡ سَبۡعَ لَيَالٖ وَثَمَٰنِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومٗاۖ فَتَرَى ٱلۡقَوۡمَ فِيهَا صَرۡعَىٰ كَأَنَّهُمۡ أَعۡجَازُ نَخۡلٍ خَاوِيَةٖ

Alio wapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani. info

Mwenyezi Mungu aliwasalitisha nao muda wa masiku saba, na siku nane zilizo fuatana mfululizo, utaona walio patikana na upepo huo wamekuwa maiti kama magogo ya mitende yaliyo kuwa matupu ndani yake. ("Masiku" ni wingi wa "Usiku"; "Siku" wingi wake ni "Siku" vile vile.)

التفاسير:

external-link copy
8 : 69

فَهَلۡ تَرَىٰ لَهُم مِّنۢ بَاقِيَةٖ

Basi je! Unamwona mmoja wao aliye baki? info

Je! Unamwona yeyote aliye bakia katika hao?

التفاسير:

external-link copy
9 : 69

وَجَآءَ فِرۡعَوۡنُ وَمَن قَبۡلَهُۥ وَٱلۡمُؤۡتَفِكَٰتُ بِٱلۡخَاطِئَةِ

Na Firauni na walio mtangulia, na miji iliyo pinduliwa chini juu, walileta khatia. info

Akaja Firauni, na mataifa mengine yaliyo kufuru kabla yake, na wale jamaa walio acha mwendo wa haki na vitendo vya maumbile wakafanya vitendo vichafu kabisa hata miji yao ikapinduliwa juu chini.

التفاسير:

external-link copy
10 : 69

فَعَصَوۡاْ رَسُولَ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَهُمۡ أَخۡذَةٗ رَّابِيَةً

Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu. info

Kila umma katika hawa walimuasi Mtume wa Mola wao Mlezi. Naye Mwenyezi Mungu akawashika kwa kuwaadhibu kwa mshiko ulio zidi ukali.

التفاسير:

external-link copy
11 : 69

إِنَّا لَمَّا طَغَا ٱلۡمَآءُ حَمَلۡنَٰكُمۡ فِي ٱلۡجَارِيَةِ

Maji yalipo furika Sisi tulikupandisheni katika safina, info

Maji yalipo zidi ukomo wake, na yakapanda juu ya milima katika tukio la tofani ya Nuhu, Sisi tulikupandisheni, yaani kwa kuwapandisha wazee wenu wa asli, katika safina inayo kwenda baharini.

التفاسير:

external-link copy
12 : 69

لِنَجۡعَلَهَا لَكُمۡ تَذۡكِرَةٗ وَتَعِيَهَآ أُذُنٞ وَٰعِيَةٞ

Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalo sikia liyahifadhi. info

Ili kulifanya tukio hilo la kuwaokoa Waumini na kuwazamisha makafiri liwe zingatio na mawaidha kwenu, na lihifadhiwe na kila sikio lenye kuhifadhi linalo sikia.

التفاسير:

external-link copy
13 : 69

فَإِذَا نُفِخَ فِي ٱلصُّورِ نَفۡخَةٞ وَٰحِدَةٞ

. Na litapo pulizwa barugumu mpulizo mmoja tu, info

Litakapo pulizwa barugumu kwa mpulizo mmoja,

التفاسير:

external-link copy
14 : 69

وَحُمِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ وَٱلۡجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةٗ وَٰحِدَةٗ

Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja, info

Na ardhi na milima ikaondolewa pahala ilipo, na ikavunjwa mara moja,

التفاسير:

external-link copy
15 : 69

فَيَوۡمَئِذٖ وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ

Siku hiyo ndio Tukio litatukia. info

Siku hiyo ndiyo kitashuka cha kushuka,

التفاسير:

external-link copy
16 : 69

وَٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَهِيَ يَوۡمَئِذٖ وَاهِيَةٞ

Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa. info

Na mbingu zitapasuka kwa kuondoka hukumu zake na sharia zake, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu baada ya kuwa madhubuti zenye nguvu.

التفاسير:

external-link copy
17 : 69

وَٱلۡمَلَكُ عَلَىٰٓ أَرۡجَآئِهَاۚ وَيَحۡمِلُ عَرۡشَ رَبِّكَ فَوۡقَهُمۡ يَوۡمَئِذٖ ثَمَٰنِيَةٞ

Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi. info

Na Malaika pembezoni mwake, na wapo Malaika wanane siku hiyo watakao beba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi, juu ya Malaika hawa wengine.

التفاسير:

external-link copy
18 : 69

يَوۡمَئِذٖ تُعۡرَضُونَ لَا تَخۡفَىٰ مِنكُمۡ خَافِيَةٞ

Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu. info

Siku hiyo ndio mtaletwa kwa ajili ya kuhisabiwa. Wala haifichikani siri yenu yoyote mliyo kuwa mkiificha.

التفاسير:

external-link copy
19 : 69

فَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ فَيَقُولُ هَآؤُمُ ٱقۡرَءُواْ كِتَٰبِيَهۡ

Basi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu! info

Ama mwenye kupewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema akiwatangazia furaha yake walio karibu naye: Chukueni msome kitabu changu!

التفاسير:

external-link copy
20 : 69

إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَٰقٍ حِسَابِيَهۡ

Hakika nalijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu. info

Mimi nilikuwa na yakini tangu duniani kuwa nitapata hisabu yangu, basi nikajitayarisha nafsi yangu kwa mkutano huu.

التفاسير:

external-link copy
21 : 69

فَهُوَ فِي عِيشَةٖ رَّاضِيَةٖ

Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza, info

Basi huyo atakuwa katika maisha yaliyo enea kupendeza.

التفاسير:

external-link copy
22 : 69

فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٖ

Katika Bustani ya juu, info

Katika Bustani ya pahali na daraja ya juu.

التفاسير:

external-link copy
23 : 69

قُطُوفُهَا دَانِيَةٞ

Matunda yake yakaribu. info

Matunda yake yakaribu kwa kuyachuma. (kuyatunda).

التفاسير:

external-link copy
24 : 69

كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَآ أَسۡلَفۡتُمۡ فِي ٱلۡأَيَّامِ ٱلۡخَالِيَةِ

Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita. info

Kuleni na mnywe kwa kula na kunywa kusio na karaha, wala maudhi, kwa sababu ya vitendo vyema mlivyo kwisha vitanguliza katika siku za duniani zilizo pita.

التفاسير:

external-link copy
25 : 69

وَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِشِمَالِهِۦ فَيَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي لَمۡ أُوتَ كِتَٰبِيَهۡ

Na ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu! info

Ama mwenye kupewa kitabu chake kwa mkono wake wa kushoto atasema kwa majuto na huzuni: Laiti kuwa sikupewa kitabu changu,

التفاسير:

external-link copy
26 : 69

وَلَمۡ أَدۡرِ مَا حِسَابِيَهۡ

Wala nisingeli jua nini hisabu yangu. info

Wala sikuijua hisabu yangu!

التفاسير:

external-link copy
27 : 69

يَٰلَيۡتَهَا كَانَتِ ٱلۡقَاضِيَةَ

Laiti mauti ndiyo yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa. info

Laiti kuwa kule kufa niliko kwisha kufa kungeli kuwa ndio kumalizika kwangu kwa mwisho, wala nisingeli fufuliwa tena!

التفاسير:

external-link copy
28 : 69

مَآ أَغۡنَىٰ عَنِّي مَالِيَهۡۜ

Mali yangu hayakunifaa kitu. info

Hapana chochote nilicho kimiliki duniani kilicho nifaa.

التفاسير:

external-link copy
29 : 69

هَلَكَ عَنِّي سُلۡطَٰنِيَهۡ

Madaraka yangu yamenipotea. info

Uzima wangu umenipotea, na nguvu zangu zimenitoka.

التفاسير:

external-link copy
30 : 69

خُذُوهُ فَغُلُّوهُ

(Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu! info

Wataambiwa walinzi wa Jahannamu: Mshikeni, na mfungeni mikono yake kwenye shingo yake.

التفاسير:

external-link copy
31 : 69

ثُمَّ ٱلۡجَحِيمَ صَلُّوهُ

Kisha mtupeni Motoni! info

Kisha msimtie popote ila ndani ya Moto wa Jahannamu,

التفاسير:

external-link copy
32 : 69

ثُمَّ فِي سِلۡسِلَةٖ ذَرۡعُهَا سَبۡعُونَ ذِرَاعٗا فَٱسۡلُكُوهُ

Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini! info

Kisha mfungeni kwenye mnyororo mrefu kabisa.

التفاسير:

external-link copy
33 : 69

إِنَّهُۥ كَانَ لَا يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ ٱلۡعَظِيمِ

Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, info

Hakika huyo alikuwa hamsadiki Mwenyezi Mungu Mtukufu,

التفاسير:

external-link copy
34 : 69

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ

Wala hahimizi kulisha masikini. info

Wala hamhimizi yoyote kuwalisha masikini.

التفاسير:

external-link copy
35 : 69

فَلَيۡسَ لَهُ ٱلۡيَوۡمَ هَٰهُنَا حَمِيمٞ

Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu, info

Basi hii leo huyu kafiri hana jamaa wa kumtetea,

التفاسير:

external-link copy
36 : 69

وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنۡ غِسۡلِينٖ

Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni. info

Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni, ambao kwa hakika ni mchanganyiko wa damu na usaha.

التفاسير:

external-link copy
37 : 69

لَّا يَأۡكُلُهُۥٓ إِلَّا ٱلۡخَٰطِـُٔونَ

Chakula hicho hawakili ila wakosefu. info

Hawakili chakula hicho ila wakosefu walio kusudia kufanya maasi yao, na wakakamia kuendelea nayo.

التفاسير:

external-link copy
38 : 69

فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَا تُبۡصِرُونَ

Basi naapa kwa mnavyo viona, info

Basi naapa kwa mnavyo viona katika vinavyo onekana,

التفاسير:

external-link copy
39 : 69

وَمَا لَا تُبۡصِرُونَ

Na msivyo viona, info

Basi naapa kwa mnavyo viona katika vinavyo onekana, na msivyo viona katika ulimwengu wa ghaibu,

التفاسير:

external-link copy
40 : 69

إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ

Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima. info

Kwamba hakika Qur'ani bila ya shaka inatoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ulimi wa Mjumbe mwenye cheo cha juu.

التفاسير:

external-link copy
41 : 69

وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَاعِرٖۚ قَلِيلٗا مَّا تُؤۡمِنُونَ

Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini. info

Wala Qur'ani si maneno ya mtunga mashairi kama mnavyo dai. Ama nyinyi ni chache mno imani yenu ya kuwa Qur'ani inatoka kwa Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
42 : 69

وَلَا بِقَوۡلِ كَاهِنٖۚ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ

Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka. info

Wala Qur'ani haisemi kwa maneno ya kumunyia munyia kama wanenavyo makuhani mlio wazoea. Ni uchache mno kukumbuka kwenu na kuzingatia khitilafu zilioko baina ya Qur'ani na maneno ya makuhani.

التفاسير:

external-link copy
43 : 69

تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. info

Hii ni uteremsho unao toka kwa Mwenye kuwaangalia walimwengu wote kwa kuwaumba na kuwalea.

التفاسير:

external-link copy
44 : 69

وَلَوۡ تَقَوَّلَ عَلَيۡنَا بَعۡضَ ٱلۡأَقَاوِيلِ

Na lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu, info

Na lau kuwa angeli dai kitu chochote ambacho tusicho kisema

التفاسير:

external-link copy
45 : 69

لَأَخَذۡنَا مِنۡهُ بِٱلۡيَمِينِ

Bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia, info

Basi bila ya shaka tungeli mshika akitoe kama mtu anavyo mkamata mtu kwa mkono wa kulia akammaliza hapo hapo.

التفاسير:

external-link copy
46 : 69

ثُمَّ لَقَطَعۡنَا مِنۡهُ ٱلۡوَتِينَ

Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo! info

Kisha bila ya shaka tungeli mkata mshipa wake wa moyo, afe saa ile ile. (Biblia inasema katika Kumbukumbu la Torati 18.20 "Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa.")

التفاسير:

external-link copy
47 : 69

فَمَا مِنكُم مِّنۡ أَحَدٍ عَنۡهُ حَٰجِزِينَ

Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeli weza kutuzuia. info

Na hapana yeyote katika nyinyi, hata ange kuwa na nguvu namna gani, angeli weza kuzuia adhabu yetu isimfikilie.

التفاسير:

external-link copy
48 : 69

وَإِنَّهُۥ لَتَذۡكِرَةٞ لِّلۡمُتَّقِينَ

Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wachamngu. info

Na hakika Qur'ani ni mawaidha kwa wanao fuata amri za Mwenyezi Mungu, na wanaepuka makatazo yake.

التفاسير:

external-link copy
49 : 69

وَإِنَّا لَنَعۡلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ

Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha. info

Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba kati yenu wapo wanao ikanusha Qur'ani.

التفاسير:

external-link copy
50 : 69

وَإِنَّهُۥ لَحَسۡرَةٌ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanao kataa. info

Na kwamba hakika hiyo bila ya shaka ni sababu ya majuto ya wanao ikataa, wakati watapo iona adhabu yao, na neema za wenye kusadiki.

التفاسير:

external-link copy
51 : 69

وَإِنَّهُۥ لَحَقُّ ٱلۡيَقِينِ

Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini. info

Na hakika Qur'ani bila ya shaka ni Haki iliyo thibiti, isiyo na shaka yoyote.

التفاسير:

external-link copy
52 : 69

فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ

Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu. info

Basi mtakase Mola wako Mlezi, na dumisha kudhukuru jina lake.

التفاسير: