Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - Bản dịch tiếng Swahili - 'Ali Muhsin Al-Barwani

external-link copy
280 : 2

وَإِن كَانَ ذُو عُسۡرَةٖ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيۡسَرَةٖۚ وَأَن تَصَدَّقُواْ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Na akiwa (mdaiwa) ana shida, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkiifanya deni kuwa ni sadaka, basi ni bora kwenu, ikiwa mnajua. [280] info

[280] Ikiwa mwenye kukopeshwa ana shida na uzito basi mpeni muhula wa kulipa deni lake mpaka wakati wa kufarijika. Na mkitoa sadaka kwa kusamehe deni au baadhi yake ni kheri yenu kama nyinyi ni watu wenye ujuzi na fahamu kuelewa maneno ya Mwenyezi Mungu anaye kufundisheni murwa na utu.

التفاسير: