Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

external-link copy
67 : 8

مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَكُونَ لَهُۥٓ أَسۡرَىٰ حَتَّىٰ يُثۡخِنَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ تُرِيدُونَ عَرَضَ ٱلدُّنۡيَا وَٱللَّهُ يُرِيدُ ٱلۡأٓخِرَةَۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

Haifai kwa Nabii awe na mateka miongoni mwa maadui wake mpaka aue kwa wingi, ili kutia kicho ndani ya nyoyo zao na aimarishe misingi ya Dini. Mnataka, enyi mkusanyiko wa Waislamu, kwa kuchukuwa kwenu fidia kutoka kwa mateka wa vita vya Badr, starehe ya ulimwenguni, na Mwenyezi Mungu Anataka kuikuza dini Yake ambayo kwayo hupatikana Akhera. Mwenyezi Mungu ni Mshindi Asiyeshindwa, ni Mwingi wa hekima katika sheria Zake. info
التفاسير: