Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

external-link copy
54 : 8

كَدَأۡبِ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمۡ فَأَهۡلَكۡنَٰهُم بِذُنُوبِهِمۡ وَأَغۡرَقۡنَآ ءَالَ فِرۡعَوۡنَۚ وَكُلّٞ كَانُواْ ظَٰلِمِينَ

Hali ya Makafiri hawa ni kama hali ya Makafiri wa jamaa za Fir'awn ambao walimkanusha Mūsā, na ni kama hali ya wale waliowakanusha Mitume wao miongoni mwa watu waliopita. Mwenyezi Mungu Aliwaangamiza kwa sababu ya madhambi yao na Akawazamisha jamaa za Fir'awn baharini. Na kila umma kati yao walikuwa wanatenda mambo ambayo haikufaa wao kuyatenda, ya kukanusha kwao Mitume wa Mwenyezi Mungu na kupinga kwao aya za Mwenyezi Mungu na kushirikisha kwao, katika ibada, asiyekuwa Yeye. info
التفاسير: