Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

external-link copy
52 : 8

كَدَأۡبِ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُ بِذُنُوبِهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ قَوِيّٞ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Hakika yale yaliyowapata washirikina siku hiyo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu katika kuwatia adabu wakiukaji mipaka miongoni mwa umma waliotangulia, mfano wa Fir'awn na waliomtangulia, walipowakanusha Mitume wa Mwenyezi Mungu na wakazipinga aya Zake. Kwa hakika Mwenyezi Mungu Aliwateremshia mateso Yake kwa sababu ya madhambi yao. Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Asiyeshindwa, ni Mkali wa mateso kwa aliyemuasi na asitubie kutokana na dhambi zake. info
التفاسير: