Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

external-link copy
49 : 8

إِذۡ يَقُولُ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ وَٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ غَرَّ هَٰٓؤُلَآءِ دِينُهُمۡۗ وَمَن يَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

Na kumbukeni waliposema watu wenye shaka na unafiki na wagonjwa wa nyoyo, huku wauona uchache wa Waislamu na wingi wa maadui wao, «Imewadanganya hawa Waislamu dini yao, ndipo ikawaingiza kwenye matatizo haya.» Na hawa wanafiki hawakuelewa kwamba mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu na akawa na uhakika wa ahadi Yake, basi Mwenyezi Mungu Hatamuacha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye ushindi, hakuna chochote kinachomshinda, ni Mwenye hekima katika uendeshaji Wake mambo na utengezaji Wake. info
التفاسير: