Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

external-link copy
48 : 8

وَإِذۡ زَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَعۡمَٰلَهُمۡ وَقَالَ لَا غَالِبَ لَكُمُ ٱلۡيَوۡمَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَإِنِّي جَارٞ لَّكُمۡۖ فَلَمَّا تَرَآءَتِ ٱلۡفِئَتَانِ نَكَصَ عَلَىٰ عَقِبَيۡهِ وَقَالَ إِنِّي بَرِيٓءٞ مِّنكُمۡ إِنِّيٓ أَرَىٰ مَا لَا تَرَوۡنَ إِنِّيٓ أَخَافُ ٱللَّهَۚ وَٱللَّهُ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Na kumbukeni pindi Shetani Alipowapambia washirikina yale waliyoyajia na waliyoyakusudia na akawaambia, «Hamuna yoyote Atakayewashinda leo, na mimi ni msaidizi wenu.» Basi yalipopambana makundi mawili: washirikina wakiwa pamoja na Shetani, na Waislamu wakiwa pamoja na Malaika, alirudi nyuma Shetani akaienda zake na akasema kuwaambia washirikina, «Mimi ni mwenye kujitenga na nyinyi; mimi nawaona Malaika msiowaona waliokuja kuwasaidia Waislamu. Hakika mimi namuogopa Mwenyezi Mungu.» Basi akawaacha na akajitenga nao. Na Mwenyezi Mungu ni Mkali wa mateso kwa aliomuasi na asitubiye toba ya kidhati. info
التفاسير: