Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

external-link copy
39 : 8

وَقَٰتِلُوهُمۡ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتۡنَةٞ وَيَكُونَ ٱلدِّينُ كُلُّهُۥ لِلَّهِۚ فَإِنِ ٱنتَهَوۡاْ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِمَا يَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Na piganeni na washirikina, enyi waumini, mpaka usiweko ushirikina na uzuiliaji wa njia ya Mwenyezi Mungu na kusiabudiwe isipokuwa Mwenyezi Mungu Peke Yake Asiye na mshirika, ili chuki ziwaondokee waja wa Mwenyezi Mungu katika ardhi na mpaka dini, utiifu na ibada vitakasiwe Mwenyezi Mungu tu bila mwingine. Wakiwa watakomeka na kuwafitini Waumini na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na wakawa kwenye dini ya haki pamoja na nyinyi, basi Mwenyezi Mungu hakifichiki Kwake wanachokifanya cha kuacha ukafiri na kuingia kwenye Uislamu. info
التفاسير: