Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

external-link copy
29 : 7

قُلۡ أَمَرَ رَبِّي بِٱلۡقِسۡطِۖ وَأَقِيمُواْ وُجُوهَكُمۡ عِندَ كُلِّ مَسۡجِدٖ وَٱدۡعُوهُ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَۚ كَمَا بَدَأَكُمۡ تَعُودُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Mola wangu Ameniamrisha usawa, na Amewaamrisha nyinyi mumtakasie ibada katika kila sehemu za ibada, hasa katika misikiti, na mumuombe Yeye hali ya kumtakasia utiifu na ibada, na muamini kufufuliwa baada ya kufa. Na kama Alivyowaleta kutoka kuwa hamkuwako,Yeye ni Muweza kuwarudishia uhai mara nyingine.» info
التفاسير: