Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

external-link copy
92 : 6

وَهَٰذَا كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ مُبَارَكٞ مُّصَدِّقُ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَلِتُنذِرَ أُمَّ ٱلۡقُرَىٰ وَمَنۡ حَوۡلَهَاۚ وَٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۖ وَهُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ يُحَافِظُونَ

Na hii Qur’ani ni Kitabu tulichokuteremshia, chenye manufaa makubwa, kinatoa ushahidi juu ya ukweli wa vitabu vilivyoteremshwa vilivyokuja kabla yake na juu ya kwamba vinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Tumekiteremsha ili uwatishie nayo, watu wa Makkah na walioko pambizoni mwake kwenye majimbo yote ya ardhi, adhabu ya Mwenyezi Mungu na mateso Yake. Na wenye kuamini uhai wa Akhera, wanaamini kwamba Qur’ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu na wanajilazimisha kusimamisha Swala kwa nyakati zake. info
التفاسير: