Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

external-link copy
57 : 6

قُلۡ إِنِّي عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَكَذَّبۡتُم بِهِۦۚ مَا عِندِي مَا تَسۡتَعۡجِلُونَ بِهِۦٓۚ إِنِ ٱلۡحُكۡمُ إِلَّا لِلَّهِۖ يَقُصُّ ٱلۡحَقَّۖ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلۡفَٰصِلِينَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Mimi niko kwenye hoja iliyo wazi ya sheria ya Mwenyezi Mungu Aliyoniletea kwa njia ya wahyi. Nayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu Peke Yake kwa ibada. Na hili mlilikanusha. Na haliko kwenye uwezo wangu jambo la kuwateremshia adhabu mnayoitaka kwa haraka. Na uamuzi wa kuchelewesha hilo uko tu kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Yeye Anahadithia ukweli na Yeye Ndiye bora wa kupambanua baina ya haki na batili kwa uamuzi Wake na hukumu Yake.» info
التفاسير: