Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

external-link copy
52 : 6

وَلَا تَطۡرُدِ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ رَبَّهُم بِٱلۡغَدَوٰةِ وَٱلۡعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجۡهَهُۥۖ مَا عَلَيۡكَ مِنۡ حِسَابِهِم مِّن شَيۡءٖ وَمَا مِنۡ حِسَابِكَ عَلَيۡهِم مِّن شَيۡءٖ فَتَطۡرُدَهُمۡ فَتَكُونَ مِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Na usiwatenge, ewe Nabii, kukaa na wewe Waislamu wanyonge wanaomuabudu Mola wao mwanzo wa mchana na mwisho wake, hali wakitaka, kwa matendo yao mema, radhi za Mwenyezi Mungu. Kitu chochote kuhusu hesabu ya maskini hawa hakiko juu yako; hesabu yao iko juu ya Mwenyezi Mungu. Na si juu yao chochote kuhusu hesabu yako. Basi ukiwatenga , utakuwa ni miongoni mwa wenye kuivuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, wenye kuweka vitu mahali pasipokuwa pake. info
التفاسير: