Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

external-link copy
50 : 6

قُل لَّآ أَقُولُ لَكُمۡ عِندِي خَزَآئِنُ ٱللَّهِ وَلَآ أَعۡلَمُ ٱلۡغَيۡبَ وَلَآ أَقُولُ لَكُمۡ إِنِّي مَلَكٌۖ إِنۡ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّۚ قُلۡ هَلۡ يَسۡتَوِي ٱلۡأَعۡمَىٰ وَٱلۡبَصِيرُۚ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Mimi sidai kuwa ninamiliki hazina za mbingu na ardhi nikawa ninazitumia nitakavyo; na sidai kuwa mimi najua al-ghayb (yasiyoonekana); na sidai kuwa mimi ni Malaika. Mimi ni Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu, nafuata yale nliyoteremshiwa kwa njia ya wahyi na nawafikishia watu wahyi Wake.» Waambie, ewe Mtume, washirikina hawa. «Je, kafiri aliye kipofu wa kutoziona aya za Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, asiziamini yuko sawa na Muumini anayeziona aya za Mwenyezi Mungu na akaziamini? Kwani nyinyi hamuzifikirii aya za Mwanye ili muione haki na muiamini?» info
التفاسير: