Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

external-link copy
46 : 6

قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِنۡ أَخَذَ ٱللَّهُ سَمۡعَكُمۡ وَأَبۡصَٰرَكُمۡ وَخَتَمَ عَلَىٰ قُلُوبِكُم مَّنۡ إِلَٰهٌ غَيۡرُ ٱللَّهِ يَأۡتِيكُم بِهِۗ ٱنظُرۡ كَيۡفَ نُصَرِّفُ ٱلۡأٓيَٰتِ ثُمَّ هُمۡ يَصۡدِفُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Nambieni ikiwa Mwenyezi Mungu Ameyaondoa masikizi yenu Akawafanya viziwi, Akayaondoa macho yenu Akawafanya vipofu na Akapiga mhuri juu ya nyoyo zenu mkawa hamufahamu neno, basi ni mola gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, awezaye kuwarudishia nyinyi vitu hivyo?» Angalia, ewe Mtume, ni namna gani sisi tunawatolea hoja aina mbalimbali, kisha wao baada yake wanakataa kukumbuka na kuzingatia? info
التفاسير: