Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

Số trang:close

external-link copy
12 : 47

إِنَّ ٱللَّهَ يُدۡخِلُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يَتَمَتَّعُونَ وَيَأۡكُلُونَ كَمَا تَأۡكُلُ ٱلۡأَنۡعَٰمُ وَٱلنَّارُ مَثۡوٗى لَّهُمۡ

Hakika Mwenyezi Mungu Atawatia, wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafanya matendo mema, kwenye mabustani ya Pepo ambayo inapita mito chini ya miti yake ikiwa ni takrima kwao. Na mfano wa wale waliokanusha katika kula kwao na kujistarehesha kwao na ulimwengu, ni kama mfano wa mifugo miongoni mwa wanyama ambao hawana hamu isipokuwa kula nyasi, hawafikirii lingine. Na Moto wa Jahanamu ndio makao yao na maskani. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 47

وَكَأَيِّن مِّن قَرۡيَةٍ هِيَ أَشَدُّ قُوَّةٗ مِّن قَرۡيَتِكَ ٱلَّتِيٓ أَخۡرَجَتۡكَ أَهۡلَكۡنَٰهُمۡ فَلَا نَاصِرَ لَهُمۡ

Na wengi miongoni mwa watu wa mijini walikuwa wana nguvu zaidi kuliko watu wa mji wako, ewe Mtume, ambao ni Makkah, waliokutoa watu wake humo. Watu wa miji hiyo tuliwaangamiza kwa adhabu za aina mbalimbali. Hawakuwa na msaidizi wa kuwanusuru kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 47

أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّهِۦ كَمَن زُيِّنَ لَهُۥ سُوٓءُ عَمَلِهِۦ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَهۡوَآءَهُم

Je yule aliyekuwa na ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ujuzi kuwa Yeye ni Mmoja, ni kama yule ambaye Shetani amempambia matendo yake maovu na akafuata yale ambayo nafsi yake ilimuita iyafuate ya kumuasi Mwenyezi Mungu na kumuabudu asiyekuwa Yeye bila ya hoja wala ushahidi? Hawalingani. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 47

مَّثَلُ ٱلۡجَنَّةِ ٱلَّتِي وُعِدَ ٱلۡمُتَّقُونَۖ فِيهَآ أَنۡهَٰرٞ مِّن مَّآءٍ غَيۡرِ ءَاسِنٖ وَأَنۡهَٰرٞ مِّن لَّبَنٖ لَّمۡ يَتَغَيَّرۡ طَعۡمُهُۥ وَأَنۡهَٰرٞ مِّنۡ خَمۡرٖ لَّذَّةٖ لِّلشَّٰرِبِينَ وَأَنۡهَٰرٞ مِّنۡ عَسَلٖ مُّصَفّٗىۖ وَلَهُمۡ فِيهَا مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ وَمَغۡفِرَةٞ مِّن رَّبِّهِمۡۖ كَمَنۡ هُوَ خَٰلِدٞ فِي ٱلنَّارِ وَسُقُواْ مَآءً حَمِيمٗا فَقَطَّعَ أَمۡعَآءَهُمۡ

Sifa ya Pepo ambayo Mwenyezi Mungu Amewaahidi wachamungu: ndani yake kuna mito mikubwa ya maji yasiyobadilika, na mito ya maziwa yasyogeuka tamu yake, na mito ya shizi ambayo wanaionea ladha wenye kuinywa, na mito ya asali iliyosafishwa isiyo na taka. Na wachamungu hawa watapata ndani ya hiyo pepo matunda yote ya aina tafauti na mengineyo. Na kubwa kuliko hayo ni kule kusitiriwa na kusamehewa dhambi zao. Basi je, wale watakaokuwa ndani ya Pepo hiyo ni kama wale watakaokaa Motoni bila kutoka humo na wakanyweshwa maji yaliyo moto sana hadi ya mwisho yakawakata tumbo zao? info
التفاسير:

external-link copy
16 : 47

وَمِنۡهُم مَّن يَسۡتَمِعُ إِلَيۡكَ حَتَّىٰٓ إِذَا خَرَجُواْ مِنۡ عِندِكَ قَالُواْ لِلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ مَاذَا قَالَ ءَانِفًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَهۡوَآءَهُمۡ

Miongoni mwa hawa wanafiki kuna wanaokusikiliza bila ya kuelewa, kwa madharau na kupuuza, mpaka wanapoondoka kutoka kwenye kikao chako, huwa wakisema wakiwaambia wale waliohudhuria kikao chako kati ya wale wenye ujuzi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa njia ya shere, «Amesema nini Muhammad hivi sasa?» Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu Amezipiga muhuri nyoyo zao, zikawa haziielewi haki wala hawaongokei kuifikia, na wakayafuata matamanio yao katika ukafiri na upotevu. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 47

وَٱلَّذِينَ ٱهۡتَدَوۡاْ زَادَهُمۡ هُدٗى وَءَاتَىٰهُمۡ تَقۡوَىٰهُمۡ

Na wale walioongoka kuifuata haki, Mwenyezi Mungu Aliwaongezea uongofu , na kwa hivyo uongofu wao ukapata nguvu na Akawaafikia kwenye uchamungu na akaufanya sahali kwao. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 47

فَهَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّا ٱلسَّاعَةَ أَن تَأۡتِيَهُم بَغۡتَةٗۖ فَقَدۡ جَآءَ أَشۡرَاطُهَاۚ فَأَنَّىٰ لَهُمۡ إِذَا جَآءَتۡهُمۡ ذِكۡرَىٰهُمۡ

Wakanushaji hawa hawangojei isipokuwa wakati wa Kiyama ambao wameahidiwa kuwa utawajia kwa ghafla. Kwani alama zake zishajitokeza na wao hawakunufaika nazo. Basi watapata wapi kukumbuka wakati wa Kiyama utakapowajia? info
التفاسير:

external-link copy
19 : 47

فَٱعۡلَمۡ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لِذَنۢبِكَ وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِۗ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مُتَقَلَّبَكُمۡ وَمَثۡوَىٰكُمۡ

Basi jua, ewe Nabii, kwamba hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na utake msamaha wa dhambi zako, na uwaombee msamaha Waumini wa kiume na Waumini wa kike. Na Mwenyezi Mungu anazijua harakati zenu mnapoangaza mchana na mahali pa kutulia kwenu mnapolala usiku. info
التفاسير: