Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

external-link copy
48 : 30

ٱللَّهُ ٱلَّذِي يُرۡسِلُ ٱلرِّيَٰحَ فَتُثِيرُ سَحَابٗا فَيَبۡسُطُهُۥ فِي ٱلسَّمَآءِ كَيۡفَ يَشَآءُ وَيَجۡعَلُهُۥ كِسَفٗا فَتَرَى ٱلۡوَدۡقَ يَخۡرُجُ مِنۡ خِلَٰلِهِۦۖ فَإِذَآ أَصَابَ بِهِۦ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦٓ إِذَا هُمۡ يَسۡتَبۡشِرُونَ

Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Anayetuma upepo ukayasukuma mawingu yaliyojaa maji, na Mwenyezi Mungu Akayasambaza mbinguni vile Anavyotaka, Akayafanya ni vipande vilivyotenganika mbalimbali, hapo ukaiona mvua inatoka mawinguni. Na Aipelekapo Mwenyezi Mungu kwa waja wake, ghafla utawakuta wameingiwa na bashasha na wanafurahi kwa kuwa Mwenyezi Mungu Amewaletea hiyo. info
التفاسير: