Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

external-link copy
42 : 30

قُلۡ سِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَٱنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلُۚ كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّشۡرِكِينَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia wenye kuyakanusha uliyokuja nayo, «Tembeeni kwenye sehemu za ardhi matembezi ya kuzingatia na kutia mambo akilini, na mtazame vile ulivyokuwa mwisho wa ummah waliopita wenye kukanusha, kama vile watu wa Nūḥ, ‘Ād na Thamūd, mtakuta kwamba mwisho wao walioishia ulikuwa mbaya zaidi na kikomo hiko walichokomea kilikuwa kibaya zaidi, kwani wengi wao walikuwa ni wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu. info
التفاسير: