Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

Số trang:close

external-link copy
126 : 20

قَالَ كَذَٰلِكَ أَتَتۡكَ ءَايَٰتُنَا فَنَسِيتَهَاۖ وَكَذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمَ تُنسَىٰ

Mwenyezi Mungu Atasema kumwambia, «Nimekufufua ukiwa kipofu, kwa kuwa wewe zilikujia aya zetu zikiwa na hoja waziwazi, ukazipa mgongo na usiziamini. Na kama ulivyoziacha ulimwenguni, basi leo vilevile utaachwa Motoni. info
التفاسير:

external-link copy
127 : 20

وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي مَنۡ أَسۡرَفَ وَلَمۡ يُؤۡمِنۢ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِۦۚ وَلَعَذَابُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَشَدُّ وَأَبۡقَىٰٓ

«Hivyo ndivyo tutakavyomtesa, kwa mateso ya hapa duniani, yule aliyepita kiasi katika kujidhulumu nafsi yake akamuasi Mola wake na asiziamini aya zake. Na kwa kweli, adhabu ya kesho Akhera waliyoandaliwa ina uchungu mkali zaidi na inadumu na kujikita zaidi, kwa kuwa haikatika na haimaliziki.» info
التفاسير:

external-link copy
128 : 20

أَفَلَمۡ يَهۡدِ لَهُمۡ كَمۡ أَهۡلَكۡنَا قَبۡلَهُم مِّنَ ٱلۡقُرُونِ يَمۡشُونَ فِي مَسَٰكِنِهِمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّأُوْلِي ٱلنُّهَىٰ

Kwani haukuwaongoza watu wako kwenye njia ya sawa, Ewe mtume, ule wingi watu waliokanusha kabala yao tuliowaangamiza na hali wao wanatembea kwenye nyumba zao na wanaziona athari za kuangamia kwao? Kwa hakika, katika wingi wa watu hao na mabaki ya adhabu waliyopewa pana mazingatio na mawaidha kwa wenye akili za kuelewa. info
التفاسير:

external-link copy
129 : 20

وَلَوۡلَا كَلِمَةٞ سَبَقَتۡ مِن رَّبِّكَ لَكَانَ لِزَامٗا وَأَجَلٞ مُّسَمّٗى

Na lau si neno litokalo kwa Mola wako na muda uliotajwa mbele Yake, wangalipata maangamivu yenye kulazimiana na wao hapa ulimwenguni, kwa kuwa wao wanastahili kuyapata kwa sababu ya ukafiri wao. info
التفاسير:

external-link copy
130 : 20

فَٱصۡبِرۡ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ قَبۡلَ طُلُوعِ ٱلشَّمۡسِ وَقَبۡلَ غُرُوبِهَاۖ وَمِنۡ ءَانَآيِٕ ٱلَّيۡلِ فَسَبِّحۡ وَأَطۡرَافَ ٱلنَّهَارِ لَعَلَّكَ تَرۡضَىٰ

Basi vumilia, ewe Mtume, juu ya yale wanayoyasema wakanushaji kuhusu wewe ya sifa mbaya na urongo, umtakase Mola wako kwa kumshukuru katika Swala ya alfajiri kabla jua halijachomoza, na katika Swala ya alasiri kabla ya jua kuzama, na katika Swala ya ishai nyakati za usiku, na umtakase Mola wako kwa kumshukuru katika Swala ya adhuhuri, kwani kipindi chake kiko nchani mwa nusu ya kwanza ya mchana na nusu ya pili, na katika Swala ya magaribi, ili ulipwe kwa matendo haya kwa namna ambayo utaridhika nayo. info
التفاسير:

external-link copy
131 : 20

وَلَا تَمُدَّنَّ عَيۡنَيۡكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعۡنَا بِهِۦٓ أَزۡوَٰجٗا مِّنۡهُمۡ زَهۡرَةَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا لِنَفۡتِنَهُمۡ فِيهِۚ وَرِزۡقُ رَبِّكَ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰ

Na usivitazame vitu ambavyo tumewastarehesha navyo hawa washirikina na wanaofanana na wao miongoni mwa aina ya starehe. Kwani hivyo ni pambo lenye kuondoka katika uhai huu wa kilimwengu. Tumewastarehesha navyo,ili tuwatahini navyo. Na riziki ya Mola wako na malipo yake ni bora kwako kuliko hivyo tulivyowastarehesha navyo na ni vya kudumu zaidi, kwani havina kukatika wala kumalizika. info
التفاسير:

external-link copy
132 : 20

وَأۡمُرۡ أَهۡلَكَ بِٱلصَّلَوٰةِ وَٱصۡطَبِرۡ عَلَيۡهَاۖ لَا نَسۡـَٔلُكَ رِزۡقٗاۖ نَّحۡنُ نَرۡزُقُكَۗ وَٱلۡعَٰقِبَةُ لِلتَّقۡوَىٰ

Na waamrishe watu wako, ewe Nabii, kuswali na ujisubirishe nayo. Sisi hatutaki kutoka kwako mali, kwani sisi ndio tunaokuruzuku na kukupa. Na mwisho mwema ulimwenguni na Akhera ni wa wachajimungu info
التفاسير:

external-link copy
133 : 20

وَقَالُواْ لَوۡلَا يَأۡتِينَا بِـَٔايَةٖ مِّن رَّبِّهِۦٓۚ أَوَلَمۡ تَأۡتِهِم بَيِّنَةُ مَا فِي ٱلصُّحُفِ ٱلۡأُولَىٰ

Na walisema wenye kukukanusha, ewe Mtume, «Basi si utuletee alama itokayo kwa Mola wako yenye kuonesha ukweli wako?» Kwani hikuwajia hii Qur’ani yenye kuisadukisha haki iliyomo kwenye Vitabu vilivyopita?» info
التفاسير:

external-link copy
134 : 20

وَلَوۡ أَنَّآ أَهۡلَكۡنَٰهُم بِعَذَابٖ مِّن قَبۡلِهِۦ لَقَالُواْ رَبَّنَا لَوۡلَآ أَرۡسَلۡتَ إِلَيۡنَا رَسُولٗا فَنَتَّبِعَ ءَايَٰتِكَ مِن قَبۡلِ أَن نَّذِلَّ وَنَخۡزَىٰ

Na lau sisi tuliwaangamiza wenye kukanusha kwa adhabu kabla hatujawapelekea Mtume na kuwateremshia Kitabu, wanagalisema, «Mola wetu! Si utuletee Mtume kutoka kwako tupate kumuamini na tufuate aya zako na Sheria yako, kabla ya sisi kudhalilika na kuhizika kwa adhabu yako.» info
التفاسير:

external-link copy
135 : 20

قُلۡ كُلّٞ مُّتَرَبِّصٞ فَتَرَبَّصُواْۖ فَسَتَعۡلَمُونَ مَنۡ أَصۡحَٰبُ ٱلصِّرَٰطِ ٱلسَّوِيِّ وَمَنِ ٱهۡتَدَىٰ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, «Kila mmoja kati yetu sisi na nyinyi anagojea matukio ya ulimengu na ni nani atakayepata ushindi na kufaulu. Basi ngojeni, mtajua ni watu gani walioko kwenye njia iliyokaa sawa na nani, kati yetu sisi na nyinyi, aliyeongoka kwenye haki.» info
التفاسير: