Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

An-Nas

external-link copy
1 : 114

قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلنَّاسِ

Sema, ewe Mtume, «Ninajilinda na kutaka hifadhi kwa Bwana wa watu, Mwenye uweza, Peke Yake, wa kulirudisha shari lao. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 114

مَلِكِ ٱلنَّاسِ

«Mfalme wa watu, Mwenye kupeleka mambo yao yote Anavyotaka, Aliye Mkwasi kutowahitajia. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 114

إِلَٰهِ ٱلنَّاسِ

«Mola wa watu, Ambaye hapana mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 114

مِن شَرِّ ٱلۡوَسۡوَاسِ ٱلۡخَنَّاسِ

«Kutokana na udhia wa shetani ambaye hutia watu wasiwasi wanapoghafilika na hujificha atajwapo Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 114

ٱلَّذِي يُوَسۡوِسُ فِي صُدُورِ ٱلنَّاسِ

«Mwenye kupenyeza shari na shaka kwenye vifua vya watu. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 114

مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ

«Miongoni mwa mashetani wa kijini na kibinadamu.» info
التفاسير: