Bản dịch ý nghĩa nội dung Qur'an - 斯瓦西里语翻译 - 阿卜杜拉·穆罕默德和纳索尔·胡麦斯

external-link copy
94 : 10

فَإِن كُنتَ فِي شَكّٖ مِّمَّآ أَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ فَسۡـَٔلِ ٱلَّذِينَ يَقۡرَءُونَ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكَۚ لَقَدۡ جَآءَكَ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ

Basi uwapo na shaka,ewe Mtume, juu ya ukweli wa yale tuliyokupa habari yake, waulize wanaosoma Kitabu kabla yako miongoni mwa watu wa Taurati na Injili. Kwani hilo limethibiti kwenye vitabu vyao. Hakika umejiwa na ukweli wa yakini, kutoka kwa Mola wako, kwamba wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na kwamba hawa Mayahudi na Wanaswara wanajua ukweli wa hilo na wanapata sifa zako katika vitabu vyao, lakini wao wanalikataa hilo pamoja na kuwa walijua. Basi usiwe ni miongoni mwa wenye kufanya shaka juu ya usawa wa hilo na ukweli wake. Makusudio ya aya hii ni kusimamisha hoja kwa washirikina kwa ushahidi wa Watu wa Kitabu kati ya Wayahudi na Wanaswara ili kuukata udhuru wao. info
التفاسير: