قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - سەۋاھىلچە تەرجىمىسى. ئەلىي مۇھسىن بەرۋانىي قىلغان

Yasin

external-link copy
1 : 36

يسٓ

Ya-Sin (Y.S.). info

Ya-Sin: Hizi ni harufi mbili zilizo anzia Sura hii kwa mujibu wa mpango wa Qur'ani katika kuanzia baadhi ya Sura kwa harufi moja moja.

التفاسير:

external-link copy
2 : 36

وَٱلۡقُرۡءَانِ ٱلۡحَكِيمِ

Kwa Haki ya Qur'ani yenye hikima! info

Ninaapa kwa Qur'ani yenye kukusanya hikima na ilimu yenye manufaa.

التفاسير:

external-link copy
3 : 36

إِنَّكَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ

Hakika wewe ni miongoni mwa walio tumwa! info

Hakika wewe, Muhammad, ni katika wale ambao Mwenyezi Mungu amewatuma kwa watu wawapelekee Uwongofu na Dini ya Haki.

التفاسير:

external-link copy
4 : 36

عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Juu ya Njia Iliyo Nyooka. info

Juu ya Njia Iliyo Sawa, nayo ndiyo Dini ya Kiislamu.

التفاسير:

external-link copy
5 : 36

تَنزِيلَ ٱلۡعَزِيزِ ٱلرَّحِيمِ

Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. info

Ni mteremsho wa Mwenye nguvu Mwenye kushinda kila kitu, ambaye hapana mtu awezae kumzuia chochote akitakacho. Mwenye kuwarehemu waja wake, kwa kuwatumia watu wa kuwaongoza njia ya kuokoka.

التفاسير:

external-link copy
6 : 36

لِتُنذِرَ قَوۡمٗا مَّآ أُنذِرَ ءَابَآؤُهُمۡ فَهُمۡ غَٰفِلُونَ

Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa , basi wao wamekuwa wenye kughafilika. info

Ili uwaonye watu ambao baba zao wa karibu hawakupata kuonywa, na kwa hivyo wamesahau yanayo wajibikia kwa Mwenyezi Mungu, na kwa nafsi zao, na kwa watu.

التفاسير:

external-link copy
7 : 36

لَقَدۡ حَقَّ ٱلۡقَوۡلُ عَلَىٰٓ أَكۡثَرِهِمۡ فَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Bila ya shaka kauli imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, kwa hivyo hawaamini. info

Sisi tulikwisha jua kuwa wengi wao hawatakhiari Imani. Basi yale tuliyo kuwa tunayajua yamewafikiana na yaliyo kwao. Basi haitakuwapo Imani kutoka kwao.

التفاسير:

external-link copy
8 : 36

إِنَّا جَعَلۡنَا فِيٓ أَعۡنَٰقِهِمۡ أَغۡلَٰلٗا فَهِيَ إِلَى ٱلۡأَذۡقَانِ فَهُم مُّقۡمَحُونَ

Tumeweka makongwa shingoni mwao, yakawafika videvuni. Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu. info

Sisi tumewafanya hao wanao kakamia juu ya ukafiri ni kama walio tiwa minyororo shingoni mwao, ikawafika videvuni mwao. Na mikono yao ikawa imefungwa kwenye vichwa vyao, vikawa vimenyanyuka juu na macho yao yameinama. Basi hawawezi kuvizungusha vichwa vyao wapate kuona.

التفاسير:

external-link copy
9 : 36

وَجَعَلۡنَا مِنۢ بَيۡنِ أَيۡدِيهِمۡ سَدّٗا وَمِنۡ خَلۡفِهِمۡ سَدّٗا فَأَغۡشَيۡنَٰهُمۡ فَهُمۡ لَا يُبۡصِرُونَ

Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao, na tumewafunika macho yao; kwa hivyo hawaoni. info

Na tumewafanya wale walio zuwiwa wasione Ishara na dalili ni kama walio fungwa baina ya kuta mbili, na macho yao yakagubikwa, wasione yaliyo mbele yao wala yaliyo nyuma yao.

التفاسير:

external-link copy
10 : 36

وَسَوَآءٌ عَلَيۡهِمۡ ءَأَنذَرۡتَهُمۡ أَمۡ لَمۡ تُنذِرۡهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Ni sawa sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini. info

Na ni sawa kwao ukiwahadharisha au ukito wahadharisha, hawaamini hao.

التفاسير:

external-link copy
11 : 36

إِنَّمَا تُنذِرُ مَنِ ٱتَّبَعَ ٱلذِّكۡرَ وَخَشِيَ ٱلرَّحۡمَٰنَ بِٱلۡغَيۡبِۖ فَبَشِّرۡهُ بِمَغۡفِرَةٖ وَأَجۡرٖ كَرِيمٍ

Hakika wewe unamwonya mwenye kufuata ukumbusho, na akamcha Arrahman, Mwingi wa Rehema, kwa ghaibu. Basi mbashirie huyo msamaha na ujira mwema. info

Hakika wanao nafiika kwa kuhadharisha kwako ni wale wanao ifuata Qur'ani na wakamkhofu Arrahman, ijapo kuwa hawamwoni. Basi watu hawa wape bishara njema kuwa Mwenyezi Mungu atawasamehe madhambi yao, na atawalipa malipo mema kwa vitendo vyao.

التفاسير:

external-link copy
12 : 36

إِنَّا نَحۡنُ نُحۡيِ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَنَكۡتُبُ مَا قَدَّمُواْ وَءَاثَٰرَهُمۡۚ وَكُلَّ شَيۡءٍ أَحۡصَيۡنَٰهُ فِيٓ إِمَامٖ مُّبِينٖ

Hakika Sisi tunawafufua wafu, na tunayaandika wanayo yatanguliza, na wanayo yaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari asli lenye kubainisha. info

Hakika Sisi tunawahuisha maiti, na tunayaandika yote waliyo yatenda na wakayakadimisha duniani, na walio yabakisha humo kuwa ni athari, mabaki, yao baada ya kufa kwao. Na kila kitu kimo katika Kitabu kilicho wazi.

التفاسير: