قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - سەۋاھىلچە تەرجىمىسى. ئەلىي مۇھسىن بەرۋانىي قىلغان

Al-Ma'un

external-link copy
1 : 107

أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يُكَذِّبُ بِٱلدِّينِ

Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo? info

Unamjua anaye kanusha malipo na hisabu ya Akhera?

التفاسير:

external-link copy
2 : 107

فَذَٰلِكَ ٱلَّذِي يَدُعُّ ٱلۡيَتِيمَ

Huyo ndiye anaye msukuma yatima, info

Ukitaka kumjua basi ni huyo ambaye anaye msukuma yatima kwa nguvu, na anamtumilia mabavu, na anamdhulumu,

التفاسير:

external-link copy
3 : 107

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ

Wala hahimizi kumlisha masikini. info

Na wala hahimizi kulishwa masikini.

التفاسير:

external-link copy
4 : 107

فَوَيۡلٞ لِّلۡمُصَلِّينَ

Basi, ole wao wanao swali, info

Maangamio yatawashukia wanao sali na wakasifika kwa sifa hizi, na wakaghafilika na Swala zao wasinafiike nazo.

التفاسير:

external-link copy
5 : 107

ٱلَّذِينَ هُمۡ عَن صَلَاتِهِمۡ سَاهُونَ

Ambao wanapuuza Sala zao; info

Maangamio yatawashukia wanao swali na wakasifika kwa sifa hizi, na wakaghafilika na Swala zao wasinafiike nazo.

التفاسير:

external-link copy
6 : 107

ٱلَّذِينَ هُمۡ يُرَآءُونَ

Ambao wanajionyesha, info

Ambao huonyesha kwa watu vitendo vyao, ili wapate cheo katika nyoyo za hao watu, na wasifiwe.

التفاسير:

external-link copy
7 : 107

وَيَمۡنَعُونَ ٱلۡمَاعُونَ

Nao huku wanazuia msaada. info

Na huku wanazuia hisani zao na msaada wao kwa watu

التفاسير: