قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - قۇرئان كەرىمنىڭ ساۋاھىلچە تەرجىمىسىنى ئابدۇللا مۇھەممەد ۋە ناسىر خەمىيس تەرجىمە قىلغان.

بەت نومۇرى:close

external-link copy
52 : 42

وَكَذَٰلِكَ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ رُوحٗا مِّنۡ أَمۡرِنَاۚ مَا كُنتَ تَدۡرِي مَا ٱلۡكِتَٰبُ وَلَا ٱلۡإِيمَٰنُ وَلَٰكِن جَعَلۡنَٰهُ نُورٗا نَّهۡدِي بِهِۦ مَن نَّشَآءُ مِنۡ عِبَادِنَاۚ وَإِنَّكَ لَتَهۡدِيٓ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Na kama vile tulivyowapelekea wahyi Manabii kabla yako wewe, ewe Nabii, tulikuletea wewe wahyi wa Qur’ani itokayo kwetu, hukuwa unajua kabla yake ni vitabu vipi vilivyotangulia wala nini Imani wala zipi Sheria zinazotokana na Mwenyezi Mungu? Lakini tumeifanya Qur’ani ni mwangaza kwa watu ambao kwa huo tunawaongoza waja wetu tunaowataka kwenye njia iliyolingana sawa. Na hakika wewe, ewe Mtume, unamuelekeza na kumuongoza kwa amri ya Mwenyezi Mungu kwenye njia iliyolingana sawa, nayo ni Uislamu, info
التفاسير:

external-link copy
53 : 42

صِرَٰطِ ٱللَّهِ ٱلَّذِي لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ أَلَآ إِلَى ٱللَّهِ تَصِيرُ ٱلۡأُمُورُ

njia ya Mwenyezi Mungu Aliye na mamlaka ya vyote vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini, hana mshirika katika hayo. Jua utanabahi kwamba kwa mwenyezi Mungu , enyi watu, yatarudi mambo yote yenu ya kheri na shari, na huko Amlipe kila mtu kwa matendo yake, yakiwa mema alipwe wema na yakiwa mabaya alipwe ubaya. info
التفاسير: