قۇرئان كەرىم مەنىلىرىنىڭ تەرجىمىسى - قۇرئان كەرىمنىڭ ساۋاھىلچە تەرجىمىسىنى ئابدۇللا مۇھەممەد ۋە ناسىر خەمىيس تەرجىمە قىلغان.

بەت نومۇرى:close

external-link copy
45 : 42

وَتَرَىٰهُمۡ يُعۡرَضُونَ عَلَيۡهَا خَٰشِعِينَ مِنَ ٱلذُّلِّ يَنظُرُونَ مِن طَرۡفٍ خَفِيّٖۗ وَقَالَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّ ٱلۡخَٰسِرِينَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ وَأَهۡلِيهِمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ أَلَآ إِنَّ ٱلظَّٰلِمِينَ فِي عَذَابٖ مُّقِيمٖ

Na utawaona, ewe Mtume, hawa madhalimu wakiorodheshwa Motoni wakiwa wadhalilifu na wanyonge, wanakutazama kwa jicho la unyonge lililo dhaifu kwa hofu waliokuwa nayo na utwevu. Na watasema waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Peponi, watakapoyaona yaliyowashukia makafiri ya hasara, «Hakika wenye hasara kikweli ni wale waliopata hasara ya nafsi zao na watu wao Siku ya Kiyama kwa kuingia Motoni.» Jua utanabahi kuwa madhalimu, siku ya Kiyama, watakuwa kwenye adhabu ya daima isiyokatika wala kuondoka. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 42

وَمَا كَانَ لَهُم مِّنۡ أَوۡلِيَآءَ يَنصُرُونَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِۗ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِن سَبِيلٍ

Na hawa wenye kukanusha, Atakapowaadhibu Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama, hawatakuwa na wasaidizi na waokozi wenye kuwanusuru kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na yoyote yule ambaye Mwenyezi Mungu Amempoteza kwa sababu ya ukanushaji wake na udhalimu, hatakuwa na njia yenye kumfikisha kwenye haki hapa duniani, na kwenye Pepo kesho Akhera, kwa kuwa yeye atakuwa amezibiwa njia za kuokoka, kwani kuongoza na kupoteza viko mkononi mwa Mwenyezi Mungu, kutakasika na kutukuka ni Kwake, na haviko kwa mwingine. info
التفاسير:

external-link copy
47 : 42

ٱسۡتَجِيبُواْ لِرَبِّكُم مِّن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَ يَوۡمٞ لَّا مَرَدَّ لَهُۥ مِنَ ٱللَّهِۚ مَا لَكُم مِّن مَّلۡجَإٖ يَوۡمَئِذٖ وَمَا لَكُم مِّن نَّكِيرٖ

Itikieni mwito wa Mola wenu, enyi wenye kukanusha, kwa kuamini na kutii kabla haijaja Siku ya Kiyama ambayo haimkiniki kuirudisha. Siku hiyo hamtakuwa na mahali pa kukimbilia penye kuwaokoa na adhabu wala mahali pa kuwasitiri mkawa hamtambulikani hapo. Katika aya hii pana dalili ya ubaya wa kuchelewesha, na pana maamrisho ya kuharakisha kufanya kila tendo zuri linalomtokea mja, kwani kuchelewesha kuna athari mbaya na vizuizi. info
التفاسير:

external-link copy
48 : 42

فَإِنۡ أَعۡرَضُواْ فَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ عَلَيۡهِمۡ حَفِيظًاۖ إِنۡ عَلَيۡكَ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُۗ وَإِنَّآ إِذَآ أَذَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِنَّا رَحۡمَةٗ فَرِحَ بِهَاۖ وَإِن تُصِبۡهُمۡ سَيِّئَةُۢ بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡ فَإِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ كَفُورٞ

Watakapokataa hawa washirikina, ewe Mtume, kumuamini Mwenyezi Mungu, basi hatukukutumiliza kuwa ni mtunzi wa matendo yao mapaka ukawa ni mwenye kuwahesabu kwa hayo. Lazima yako haikuwa isipokuwa ni kufikisha ujumbe. Na sisi tunapompa binadamu rehema kutoka kwetu rehema ya utajiri, ukunjufu wa mali na mengineyo, hufurahika na akapendezwa, na unapowakumba msiba wa umasikini, ugonjwa na mengineyo kwa sababu ya kile kilichotangulizwa na mikono yao cha kufanya matendo ya kumuasi Mwenyezi Mungu, hapo binadamu huwa ni mwenye kukataa sana, huwa akihesabu misiba na akisahau neema. info
التفاسير:

external-link copy
49 : 42

لِّلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُۚ يَهَبُ لِمَن يَشَآءُ إِنَٰثٗا وَيَهَبُ لِمَن يَشَآءُ ٱلذُّكُورَ

Ni ya Mwenyezi Mungu mamlaka ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Anaumba viumbe anavyovitaka. Anamtunuku Anayemtaka miongoni mwa waja Wake wanawake bila kuwa na wanaume pamoja nao, na Anamtunuku Anayemtaka wanaume bila kuwa na wanawake pamoja nao. info
التفاسير:

external-link copy
50 : 42

أَوۡ يُزَوِّجُهُمۡ ذُكۡرَانٗا وَإِنَٰثٗاۖ وَيَجۡعَلُ مَن يَشَآءُ عَقِيمًاۚ إِنَّهُۥ عَلِيمٞ قَدِيرٞ

Na Anampa, Anayetakasika na kutukuka, Anayemtaka miongoni mwa watu wanaume na wanawake. Na Anamfanya Anayemtaka kuwa tasa asiyezaa. Hakika Yeye ni Mjuzi sana wa Anachoumba, ni Muweza sana kuumba Anachotaka, hakuna chochote kinachomshinda Akitaka kukiumba. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 42

۞ وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ ٱللَّهُ إِلَّا وَحۡيًا أَوۡ مِن وَرَآيِٕ حِجَابٍ أَوۡ يُرۡسِلَ رَسُولٗا فَيُوحِيَ بِإِذۡنِهِۦ مَا يَشَآءُۚ إِنَّهُۥ عَلِيٌّ حَكِيمٞ

Na haipasi kwa kiumbe yoyote, kati ya binadamu, Mwenyezi Mungu Aseme naye isipokuwa kwa njia ya wahyi ambao Mwenyezi Mungu Anamtumia au Aseme naye nyuma ya pazia, kama vile Alivyosema Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, na Mūsā, amani imshukie, Au Atume mjumbe, kama Anavoyomtuma Jibrili, amani imshukie, kwa yule anayetumwa kwake ampelekee wahyi wa kile Mwenyezi Mungu Anataka apelekewe, kwa idhini ya Mola wake, na sio kwa mapendeleo yake. Hakika Yake Yeye, Aliyetukuka, Yuko juu kwa dhati Yake, majina Yake, sifa Zake na vitendo Vyake. Amekilazimisha kila kitu, na viumbe vyote vimemdhalilikia, ni Mwingi wa hekima katika uedeshaji Wake mambo ya viumbe Vyake. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya kusema kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa namna inayonasibiana na haiba Yake na ukubwa wa mamlaka Yake. info
التفاسير: