Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili ni Ali Mohsin Al-Barwani

Numero ng Pahina:close

external-link copy
127 : 2

وَإِذۡ يَرۡفَعُ إِبۡرَٰهِـۧمُ ٱلۡقَوَاعِدَ مِنَ ٱلۡبَيۡتِ وَإِسۡمَٰعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلۡ مِنَّآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi. info

Na alipo kuwa Ibrahim na mwanawe Ismail wananyanyua misingi ya Alkaaba na huku wakimwomba Mwenyezi Mungu: Mola Mlezi wetu, Ewe Muumba wetu, na Muanzishi wetu! Tupokelee hii kazi yetu tuifanyayo kwa usafi wa niya kwa ajili yako, kwani Wewe ni Mwenye kusikia maombi yetu, ni Mwenye kujua ukweli wa niya yetu.

التفاسير:

external-link copy
128 : 2

رَبَّنَا وَٱجۡعَلۡنَا مُسۡلِمَيۡنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَآ أُمَّةٗ مُّسۡلِمَةٗ لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبۡ عَلَيۡنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ

Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. info

Mola Mlezi wetu! Tuwezeshe na utujaalie tuwe wenye kukusafia niya Wewe, na miongoni mwa vizazi vyetu wajaalie watoke watu wenye kukusafia Wewe. Na tufundishe njia za ibada yetu kukuabudu Wewe katika Nyumba hii takatifu na pembezoni mwake, na pokea toba yetu tunapo sahau au tunapo kosea. Hakika Wewe ni mwingi wa kupokea toba za waja wako, na Msamehevu kwao kwa fadhila yako na rehema yako.

التفاسير:

external-link copy
129 : 2

رَبَّنَا وَٱبۡعَثۡ فِيهِمۡ رَسُولٗا مِّنۡهُمۡ يَتۡلُواْ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَيُزَكِّيهِمۡۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. info

Mola Mlezi wetu! Waletee kutokana na vizazi vyetu Mtume miongoni mwao atakaye wasomea Aya zako na atawafundisha yale utakayo mfunulia yeye katika Kitabu na ilimu zenye manufaa na sharia zenye hikima, na awatakase kutokana na tabia mbovu. Hakika Wewe ndiye Mwenye kushinda, Mwenye nguvu, Mwenye hikima katika uyatendayo na unayo yaamrisha na unayo yakataza. Mwenyezi Mungu hakupeleka Mtume kutokana na vizazi vya Ismail ila Muhammad s.a.w. Kwake yeye ndiyo dua hii imepokelewa na Mwenyezi Mungu kwa kutumwa kwa vizazi vya Ismaili na wanaadamu wote.

التفاسير:

external-link copy
130 : 2

وَمَن يَرۡغَبُ عَن مِّلَّةِ إِبۡرَٰهِـۧمَ إِلَّا مَن سَفِهَ نَفۡسَهُۥۚ وَلَقَدِ ٱصۡطَفَيۡنَٰهُ فِي ٱلدُّنۡيَاۖ وَإِنَّهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ لَمِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema. info

Aliyo yafanya Ibrahim na aliyo yaomba kwa Mwenyezi Mungu ni mambo mazuri mno. Hali kadhaalika mila aliyo ifuata ni mila iliyo kwenda sawa kabisa. Na hapana anaye jitenga na mila ya Ibrahim ila mwenye kuudharau utu wake mwenyewe na akili yake. Hakika Mwenyezi Mungu alimteuwa yeye Ibrahim katika dunia, na pia Akhera ni miongoni mwa watu wema walio karibishwa.

التفاسير:

external-link copy
131 : 2

إِذۡ قَالَ لَهُۥ رَبُّهُۥٓ أَسۡلِمۡۖ قَالَ أَسۡلَمۡتُ لِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote. info

Yeye Ibrahim aliitikia amri ya Mola wake Mlezi pale alipo mtaka asilimu, yaani anyenyekee. Akasema: Namnyenyekea Mola Mlezi wa walimwengu wote, majini, watu na Malaika.

التفاسير:

external-link copy
132 : 2

وَوَصَّىٰ بِهَآ إِبۡرَٰهِـۧمُ بَنِيهِ وَيَعۡقُوبُ يَٰبَنِيَّ إِنَّ ٱللَّهَ ٱصۡطَفَىٰ لَكُمُ ٱلدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسۡلِمُونَ

Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu. info

Na Ibrahim hakutosheka na hayo tu, bali aliwausia wanawe wende mwendo wa uwongofu kama wake. Na mjukuu wake Yaakubu akamuiga, naye akawausia wanawe kadhaalika wafuate mwenendo huo huo. Aliwabainishia wanawe ya kwamba Mwenyezi Mungu amewateulia Dini ya Tawhidi, ya Mungu Mmoja. Na akachukua kwao ahadi kuwa hawatakufa ila nao ni Waislamu, wenye kuthibiti juu ya Dini hii.

التفاسير:

external-link copy
133 : 2

أَمۡ كُنتُمۡ شُهَدَآءَ إِذۡ حَضَرَ يَعۡقُوبَ ٱلۡمَوۡتُ إِذۡ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعۡبُدُونَ مِنۢ بَعۡدِيۖ قَالُواْ نَعۡبُدُ إِلَٰهَكَ وَإِلَٰهَ ءَابَآئِكَ إِبۡرَٰهِـۧمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ إِلَٰهٗا وَٰحِدٗا وَنَحۡنُ لَهُۥ مُسۡلِمُونَ

Je! Mlikuwapo yalipo mfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu Mmoja tu, na sisi tunasilimu kwake. info

Na nyinyi Mayahudi mlidai kuwa nyinyi mnakwenda mwendo wa Dini aliyo kufa nayo Yaakubu. Kwani nyinyi mlikuwapo pale mauti yalipo mjia Yaakubu hata mkajua kuwa alikufa katika mila gani? Basi zindukaneni mjue ya kuwa Yaakubu na wanawe walikuwa Waislamu wenye kumuamini Mungu Mmoja, wala wao hawakuwa Mayahudi kama nyinyi, wala hawakuwa Wakristo. ("Uyahudi" umeanza kuitwa hivyo baada ya Yuda, mwana wa Yaakubu. "Ukristo" ni baada ya Isa Masihi, Yesu Kristo. Ama "Uislamu", yaani unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, ni Dini ya maumbile, ipo milele.) Na mjue ya kuwa Yaakubu alipo kabiliwa na mauti aliwakusanya wanawe na akawaambia: Mtaabudu nini baada yangu? Na wao wakajibu: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako Ibrahim na Ismail na Is-hak, Mungu Mmoja; na kwake Yeye tunanyenyekea.

التفاسير:

external-link copy
134 : 2

تِلۡكَ أُمَّةٞ قَدۡ خَلَتۡۖ لَهَا مَا كَسَبَتۡ وَلَكُم مَّا كَسَبۡتُمۡۖ وَلَا تُسۡـَٔلُونَ عَمَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Hao ni watu walio kwisha pita. Watapata waliyo yachuma, nanyi mtapata mtakayo yachuma; wala hamtaulizwa nyinyi waliyo kuwa wakiyafanya wao. info

Tena imekuwaje enyi Mayahudi kujadili mambo ya watu hawa? Hao ni watu walio kwisha pita na njia yao. Tena wao peke yao watavuna yale waliyo yatenda katika maisha yao. Nyinyi, basi, hamtaulizwa kitu juu ya vitendo vyao, na wala nyinyi hamtapata faida yoyote katika hayo. Nanyi hamtavuna ila yale matunda ya vitendo vyenu mnavyo vitenda nyinyi wenyewe.

التفاسير: