แปล​ความหมาย​อัลกุรอาน​ - คำแปลภาษาสวาฮิลี - อะลีย์ มุห์สิน อัลบัรวานีย์

Al-Fil

external-link copy
1 : 105

أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصۡحَٰبِ ٱلۡفِيلِ

Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo? info

Hakika, ewe Muhammad, unajua kwa ujuzi usio ingiliwa na shaka yoyote, alivyo fanya Mola wako Mlezi kuwafanyia wale watu wenye tembo (ndovu), wakataka kuishambulia Nyumba takatifu ya Al-Kaaba.

التفاسير:

external-link copy
2 : 105

أَلَمۡ يَجۡعَلۡ كَيۡدَهُمۡ فِي تَضۡلِيلٖ

Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika? info

Unajua ya kwamba hakika Mwenyezi Mungu amejaalia juhudi yao kutaka kuibomoa Al-Kaaba ivize na ipotelee mbali. Juhudi yao ikapeperuka, na wao wasipate makusudio yao.

التفاسير:

external-link copy
3 : 105

وَأَرۡسَلَ عَلَيۡهِمۡ طَيۡرًا أَبَابِيلَ

Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi, info

Na Mwenyezi Mungu aliwasalitisha na majeshi ya ndege yaliyo watokea makundi kwa makundi yakifuatana, na yakawazunguka kila upande.

التفاسير:

external-link copy
4 : 105

تَرۡمِيهِم بِحِجَارَةٖ مِّن سِجِّيلٖ

Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni, info

Wakiwatupia mawe kutoka Jahannamu.

التفاسير:

external-link copy
5 : 105

فَجَعَلَهُمۡ كَعَصۡفٖ مَّأۡكُولِۭ

Akawafanya kama majani yaliyo liwa! info

Akawafanya kama majani ya mimea yaliyo sibiwa yakatilifu.

التفاسير: