แปล​ความหมาย​อัลกุรอาน​ - คำแปลภาษาสวาฮิลี - อับดุลลอฮ์ มุฮัมมัด และ นาศิร เคาะมีส

Al-Qiyamah

external-link copy
1 : 75

لَآ أُقۡسِمُ بِيَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ

Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Siku ya Hesabu na Malipo, info
التفاسير:

external-link copy
2 : 75

وَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلنَّفۡسِ ٱللَّوَّامَةِ

na Anaapa kwa nafsi yenye kuamini na kuchamungu, inayomlaumu mwenyewe kwa kuacha matendo ya utiifu na kufanya matendo yenye kuangamiza, kwamba watu watafufuliwa. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 75

أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَلَّن نَّجۡمَعَ عِظَامَهُۥ

Je anadhanihuyu binadamu kafiri kuwa sisi hatutaweza kuikusanya mifupa yake baada ya kuwa mbalimbali.? info
التفاسير:

external-link copy
4 : 75

بَلَىٰ قَٰدِرِينَ عَلَىٰٓ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُۥ

Ndio! Tutaikusanya na tunaweza kufanya vidole vyake au ncha za vidole vyake- baada ya kuvikusanya na kuzioanisha- viwe kwenye umbo la sawasawa, kama vilivyokuwa kabla ya kufa. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 75

بَلۡ يُرِيدُ ٱلۡإِنسَٰنُ لِيَفۡجُرَ أَمَامَهُۥ

Bali binadamu anakanusha kufufuliwa, anataka asalie kwenye kufanya ubaya kwa siku za mbeleni za maisha yake. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 75

يَسۡـَٔلُ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلۡقِيَٰمَةِ

Kafiri huyu huwa akiuliza, akiliona jambo la kusimama Kiyama kuwa liko mbali, «Ni lini Siku ya Kiyama?’ info
التفاسير:

external-link copy
7 : 75

فَإِذَا بَرِقَ ٱلۡبَصَرُ

Basi macho yatakapoduwaa na yakashituka kwa kutishika na kile yalichokiona cha vituko vya Siku ya Kiyama, info
التفاسير:

external-link copy
8 : 75

وَخَسَفَ ٱلۡقَمَرُ

na ukafutika mwangaza wa mwezi, info
التفاسير:

external-link copy
9 : 75

وَجُمِعَ ٱلشَّمۡسُ وَٱلۡقَمَرُ

na vikakusanywa jua na mwezi katika kukosa mwangaza, kikawa kila mojawapo ya hivyo viwili hakina mwangaza, info
التفاسير:

external-link copy
10 : 75

يَقُولُ ٱلۡإِنسَٰنُ يَوۡمَئِذٍ أَيۡنَ ٱلۡمَفَرُّ

wakati huo binadamu atasema, «Pa kukimbilia ni wapi kuiepuka adhabu?» info
التفاسير:

external-link copy
11 : 75

كَلَّا لَا وَزَرَ

Mambo sivyo kama unavyotamani yawe, ewe binadamu, ya kutaka kukimbia. Huna mahali pa kukimbilia wala pa kupata uokozinfsi yake. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 75

إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡمُسۡتَقَرُّ

Kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake ndio mwisho wa viumbe Siku ya Kiyama na ndipo mahali pao pa kutulia, na hapo Amlipe kila mtu kwa kile alichostahiki. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 75

يُنَبَّؤُاْ ٱلۡإِنسَٰنُ يَوۡمَئِذِۭ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ

Atapashwa habari binadamu Siku hiyo kwa matendo yake yote, mema na mabaya, aliyoyatanguliza miongoni mwa hayo katika maisha yake na aliyoyachelewesha. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 75

بَلِ ٱلۡإِنسَٰنُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ بَصِيرَةٞ

Bali binadamu ni hoja iliyo wazi juu ya nafsi yake, yenye kumfuata kwa alichokitenda na alichokiacha, info
التفاسير:

external-link copy
15 : 75

وَلَوۡ أَلۡقَىٰ مَعَاذِيرَهُۥ

hata kama atakuja na kila udhuru wa kuelezea sababu ya uhalifu wake, hilo halitamfaa. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 75

لَا تُحَرِّكۡ بِهِۦ لِسَانَكَ لِتَعۡجَلَ بِهِۦٓ

Usitikise, ewe Nabii, ulimi wako kwa Qur’ani wakati wahyi unapoteremka ili ufanye haraka kuihifadhi kwa kuogopa isikuponyoke. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 75

إِنَّ عَلَيۡنَا جَمۡعَهُۥ وَقُرۡءَانَهُۥ

Kwani ni juu yetu sisi kuikusanya kwenye kifua chako kisha uisome kwa ulimi wako wakati utakapo. Mjumbe wetu Jibrili akikusomea, info
التفاسير:

external-link copy
18 : 75

فَإِذَا قَرَأۡنَٰهُ فَٱتَّبِعۡ قُرۡءَانَهُۥ

basi kisikilize kisomo chake na umpulikize. Kisha isome kama alivyokusomea, info
التفاسير:

external-link copy
19 : 75

ثُمَّ إِنَّ عَلَيۡنَا بَيَانَهُۥ

kisha ni juu yetu kukuelezea kilichokutatiza kukifahamu katika maana yake na hukumu zake. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 75

كَلَّا بَلۡ تُحِبُّونَ ٱلۡعَاجِلَةَ

Mambo sivyo kama mlivyodai, enyi mkusanyiko wa washirikina, kuwa hakuna kufufuliwa wala kulipwa. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 75

وَتَذَرُونَ ٱلۡأٓخِرَةَ

Bali nyinyi ni watu mnaopenda dunia na pambo lake na mnaacha Akhera na starehe zake. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 75

وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ نَّاضِرَةٌ

Nyuso za watu wema Siku ya Kiyama zitakuwa ni zenye kung’ara, nzuri na zenye furaha, info
التفاسير:

external-link copy
23 : 75

إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٞ

zitamuona Mola Aliyeziumba na Anayezimiliki, na zitastarehe kwa hilo. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 75

وَوُجُوهٞ يَوۡمَئِذِۭ بَاسِرَةٞ

Nyuso za watu wabaya Silku ya Kiyama zitakuwa ni zenye kukunjana na kusinyaa, info
التفاسير:

external-link copy
25 : 75

تَظُنُّ أَن يُفۡعَلَ بِهَا فَاقِرَةٞ

zinatazamia kushukiwa na msiba mkubwa wenye kuvunja. info
التفاسير:

external-link copy
26 : 75

كَلَّآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلتَّرَاقِيَ

Ni kweli! Pindi roho itakapofika sehemu za juu za kifua, info
التفاسير:

external-link copy
27 : 75

وَقِيلَ مَنۡۜ رَاقٖ

na wakasema baadhi ya waliohudhuria kuwaambia wengine, «Je kuna mtu wa kumzungua na kumpoza kutokana na hali hii aliyonayo?» info
التفاسير:

external-link copy
28 : 75

وَظَنَّ أَنَّهُ ٱلۡفِرَاقُ

Na yule ambaye yuko katika hali ya kufa akajua kwamba lile lililomshukia ni kuaga dunia, kwa kuwa anawaona Malaika wa mauti. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 75

وَٱلۡتَفَّتِ ٱلسَّاقُ بِٱلسَّاقِ

Na ikashikana shida ya mwisho wa duniani na shida ya mwanzo wa Akhera. Kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. info
التفاسير:

external-link copy
30 : 75

إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡمَسَاقُ

Watu watapelekwa Siku ya Kiyama: ima Peponi au Motoni. info
التفاسير:

external-link copy
31 : 75

فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ

Hakuwa kafiri ni mwenye kumuamini Mtume na Qur’ani, wala hakuwa ni mwenye kumtekelezea Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Swala za faradhi. info
التفاسير:

external-link copy
32 : 75

وَلَٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ

Lakini aliikanusha Qur’ani na akaipa mgongo Imani, info
التفاسير:

external-link copy
33 : 75

ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ يَتَمَطَّىٰٓ

kisha akaenda kwa watu wake akijiona hali ya kujigamba katika kutembea kwake. Basi maangamivu info
التفاسير:

external-link copy
34 : 75

أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰ

ni yako baada ya maangamivu! info
التفاسير:

external-link copy
35 : 75

ثُمَّ أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰٓ

Kisha maangamivu ni yako baada ya maangamivu! info
التفاسير:

external-link copy
36 : 75

أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَن يُتۡرَكَ سُدًى

Je anadhani huyu binadamu anayekanusha kufufuliwa kuwa ataachwa bure: haamrishwi wala hakatazwi, hahesabiwi wala hateswi? info
التفاسير:

external-link copy
37 : 75

أَلَمۡ يَكُ نُطۡفَةٗ مِّن مَّنِيّٖ يُمۡنَىٰ

Kwani hakuwa binadamu huyu ni tone la manii dhaifu linalotokana na maji matwevu yanayomwagwa na kumiminwa kwenye kizazi, info
التفاسير:

external-link copy
38 : 75

ثُمَّ كَانَ عَلَقَةٗ فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ

kisha yakawa ni kipande cha damu iliyo kavu. Mwenyezi Mungu Akaliumba kwa uweza Wake na Akazilinganisha sura zake katika umbo la mwili lililo zuri kabisa? info
التفاسير:

external-link copy
39 : 75

فَجَعَلَ مِنۡهُ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ

Akafanya kutokana na binadamu huyu jinsi mbili: ya kiume na ya kike. Je kwani hakuwa Mola huyo Muumba wa vitu hivyo ni Muweza wa kuwarudisha viumbe wakiwa hai baada ya kutoweka kwao. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 75

أَلَيۡسَ ذَٰلِكَ بِقَٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يُحۡـِۧيَ ٱلۡمَوۡتَىٰ

Ndio! Anaweza. Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, kwa hakika ni Muweza wa hilo. info
التفاسير: