Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Ali Muhsin el-Beruani

Ad-Duha

external-link copy
1 : 93

وَٱلضُّحَىٰ

Naapa kwa mchana! info

Naapa kwa wakati wa kupanda juu jua, na ni wakati wa uchangamfu na kazi!

التفاسير:

external-link copy
2 : 93

وَٱلَّيۡلِ إِذَا سَجَىٰ

Na kwa usiku unapo tanda! info

Na naapa kwa usiku unapo tulia na ukatanda kote kiza chake!

التفاسير:

external-link copy
3 : 93

مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ

Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe. info

Ewe Muhammad! Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukuchukia.

التفاسير:

external-link copy
4 : 93

وَلَلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لَّكَ مِنَ ٱلۡأُولَىٰ

Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia. info

Na matokeo ya mambo yako, mwisho wake, yatakuwa bora kuliko mwanzo wake.

التفاسير:

external-link copy
5 : 93

وَلَسَوۡفَ يُعۡطِيكَ رَبُّكَ فَتَرۡضَىٰٓ

Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike. info

Na ninaapa kuwa bila ya shaka hapo Mola wako Mlezi atakupa kheri za duniani na Akhera hata utaridhia.

التفاسير:

external-link copy
6 : 93

أَلَمۡ يَجِدۡكَ يَتِيمٗا فَـَٔاوَىٰ

Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi? info

Kwani hakukukuta wewe yatima unahitaji wa kukutunza naye akakupa makaazi ya kukuhifadhi kwa mwenye kukuangalia vyema kwa mambo yako?

التفاسير:

external-link copy
7 : 93

وَوَجَدَكَ ضَآلّٗا فَهَدَىٰ

Na akakukuta umepotea akakuongoa? info

Na akakuona umebabaika hukukinaika na itikadi zilizo kuzunguka, naye akakuongoa kwenye Njia ya Haki?

التفاسير:

external-link copy
8 : 93

وَوَجَدَكَ عَآئِلٗا فَأَغۡنَىٰ

Akakukuta mhitaji akakutosheleza? info

Akakukuta fakiri wa mali naye akakutajirisha kwa kukupa riziki?

التفاسير:

external-link copy
9 : 93

فَأَمَّا ٱلۡيَتِيمَ فَلَا تَقۡهَرۡ

Basi yatima usimwonee! info

Ikiwa hii ndiyo hali yetu nawe, basi yatima usimdhili,

التفاسير:

external-link copy
10 : 93

وَأَمَّا ٱلسَّآئِلَ فَلَا تَنۡهَرۡ

Na anaye omba au kuuliza usimkaripie! info

Na mwenye kuomba au kuuliza usimjibu kwa ukavu,

التفاسير:

external-link copy
11 : 93

وَأَمَّا بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثۡ

Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie. info

Na ama neema za Mola wako Mlezi zitangaze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa ndio kudhihirisha neema.

التفاسير: