Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Ali Muhsin el-Beruani

external-link copy
102 : 9

وَءَاخَرُونَ ٱعۡتَرَفُواْ بِذُنُوبِهِمۡ خَلَطُواْ عَمَلٗا صَٰلِحٗا وَءَاخَرَ سَيِّئًا عَسَى ٱللَّهُ أَن يَتُوبَ عَلَيۡهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ

Na wengine walikiri dhambi zao, wakachanganya vitendo vyema na vingine viovu. Asaa Mwenyezi Mungu akapokea toba zao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. [102] info

[102] Na wapo watu wengine walio kuudhini, kisha baadae wakakubali makosa yao, na wakafuata Njia ya Haki. Basi watu hao wamefanya vitendo vyema na vitendo viovu. Kwa hao inatarajiwa kukubaliwa toba yao. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemu waja wake; huikubali toba yao na huwasamehe.

التفاسير: